Aug 19, 2017 14:57 UTC
  • Wapinzani Uturuki: Chama cha Rais Tayyip Erdoğan hakina tofauti na Daesh

Wapinzani wa serikali ya Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki wamekosoa misimamo ya kiongozi huyo kuhusiana na suala la kulinda turathi za kihistoria na kuongeza kuwa, serikali ya nchi hiyo haina tofauti na makundi ya kigaidi na ukufurishaji hususan Daesh.

Mwakilishi wa chama cha Demokrasia ya Watu wa Uturuki amesema kuwa, serikali ya chama tawala inayoongozwa na Rais Recep Tayyip Erdoğan na kundi la Daesh ni pande mbili za sarafu moja. Muhammad Ali Aslan amesema kuwa, serikali ya chama tawala nchini humo inafuata misimamo na idolojia zile zile za kundi la kigaidi na la Daesh (ISIS). 

Sehemu ya turahi za kihistoria zilizoharibiwa na magaidi wa Daesh

Ali Aslan ameongeza kuwa, hakuna tofauti yoyote kati ya serikali ya Erdoğan inayokusudia kuharibu turathi za kihistoria za Uturuki kwa kisingizio kuwa turathi hizo ziko katika mkondo wa mto wa Tigris, na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh ambalo linaharibu kila uchao turathi za kihistoria katika maeneo linayoyadhibiti.

Kufuatia hali hiyo, Muhammad Ali Aslan amelitaka Shirika la Elimu, Syansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuingilia kati suala hilo kwa lengo la kuizuia serikali ya Rais Recep Tayyip Erdoğan kutekeleza mpango huo haribifu katika mji wa Mardin, kusini mashariki mwa Uturuki.

Magaidi wa kundi la Daesh 

Ripoti zinasema, turathi hizo za kihistoria ambazo zimepangwa kuharibiwa na serikali, zina umri wa miaka 2500.

Tags