Madhara ya kuenezwa chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33738-madhara_ya_kuenezwa_chuki_dhidi_ya_uislamu_barani_ulaya
Kuongezeka wimbi la vyombo vya habari vinavyoeneza chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya kumewaweka katika wakati mgumu sana Waislamu barani humo kiasi kwamba uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa, kati ya kila watu watano wa barani Ulaya, mmoja anachukia kuwa na jirani Muislamu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 28, 2017 15:30 UTC
  • Madhara ya kuenezwa chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya

Kuongezeka wimbi la vyombo vya habari vinavyoeneza chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya kumewaweka katika wakati mgumu sana Waislamu barani humo kiasi kwamba uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa, kati ya kila watu watano wa barani Ulaya, mmoja anachukia kuwa na jirani Muislamu.

Mtandao wa televisheni ya Russia Today umenukuu matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyofanywa na taasisi ya Brölsmann ya nchini Ujerumani mwaka huu wa 2017 ambao umeshirikisha watu elfu 10 kutoka Ujerumaini, Austria, Uswisi, Ufaransa na Uingereza na kuongeza kuwa, asilimia 20 ya watu walioshiriki kwenye uchunguzi huo hawataki kabisa kuwa na jirani Muislamu. Ikumbukwe kuwa kuna karibu Waislamu milioni 14 katika nchi hizo tano za Ulaya.

Wanafunzi Waislamu barani Ulaya

 

Matokeo ya uchunguzi wa taasisi hiyo ya Kijerumaini unaonesha kuwa chuki dhidi ya Uislamu ziko juu kwa asilimia 28 nchini Austria huku Ufaransa ikiwa ndiyo nchi yenye kiwango cha chini zaidi ya chuki hizo kati ya nchi hizo tano za Ulaya kwa kuwa na asilimia 14 ya chuki dhidi ya Uislamu.

Uchunguzi huo umeonesha kuwa, asilimia 31 ya wananchi wa nchi hizo tano za Ulaya hawataki kabisa kuwa karibu na wahamiaji bila ya kujali itikadi za kidini za wahamiaji hao.

Kwa mujibu wa taasisi hiyo ya uchunguzi wa maoni ya Brölsmann, kuna ubaguzi mkubwa dhidi ya Waislamu katika soko la ajira barani Ulaya na kwamba ubaguzi huo hauishii katika uajiri tu, bali hata katika mishahara. Kwa mfano nchini Ujerumaini Waislamu wanalipwa mishahara ya chini sana na wanatumiwa katika kazi zenye mishahara midogo ambazo watu wengine wanakwepa kuzifanya.