Marekani yahamakishwa na kufeli njama zake dhidi ya Iran
-
Sarah Huckabee Sanders, msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House
Baada ya kushindwa njama zake zote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, msemaji wa Ikulu ya Marekani White House amemalizia hamaki zake kwa kudai kuwa eti Iran inasababisha matatizo duniani.
Shirika la habari la IRIB limemnukuu Sarah Huckabee Sanders akitoa hamaki zake hizo jana Ijumaa mbele ya waandishi wa habari na kudai kuwa, rais wa Marekani, Donald Trump anafuatilia kwa karibu kile alichodai mienendo yote mibaya ya Iran.

Msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani amedai pia kuwa, Trump anafuatilia kwa karibu makubaliano ya nyuklia na Iran, siasa za Iran za kujiimarisha kwa makombora, mashambulizi ya mitandao pamoja na miradi ya nyuklia ya Iran.
Madai hayo ya msemaji wa Ikulu ya Marekani yametolewa katika hali ambayo hivi sasa serikali ya Trump imehamikishwa sana na kufeli njama zake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la kiistratijia la magharibi mwa Asia.
Siasa imara za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimevuruga njama za miaka kadhaa za Wamarekani katika eneo hili.