Russia yawaonya raia wake kutotembelea Ulaya na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i36484-russia_yawaonya_raia_wake_kutotembelea_ulaya_na_marekani
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imewatahadharisha raia wake walio na nia ya kutembelea Marekani na nchi za Ulaya katika kipindi cha sherehe za mwaka mpya wa Milaadia na kusema kuwa kuna hatari ya kutokea mashambulizi ya kigaidi katika nchi hizo.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Nov 18, 2017 15:20 UTC
  • Russia yawaonya raia wake kutotembelea Ulaya na Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imewatahadharisha raia wake walio na nia ya kutembelea Marekani na nchi za Ulaya katika kipindi cha sherehe za mwaka mpya wa Milaadia na kusema kuwa kuna hatari ya kutokea mashambulizi ya kigaidi katika nchi hizo.

Kitengo cha kufuatilia migogoro cha wizara ya mambo ya nje ya Russia kimetoa onyo maalumu leo Jumamosi na kuwataka raia wake wenye nia ya kutembelea nchi za Ulaya na Marekani wakati wa sherehe za X-Mass kuacha kufanya hivyo.

Tamko la wizara ya mambo ya nje ya Russia limesema, kuna hatari ya kutokea mashambulizi ya kigaidi katika miji mikubwa ya Ulaya na Marekani wakati wa sherehe za mwaka mpya zinazoanza tarehe 20 Disemba na kuendelea hadi tarehe 20 Januari, hivyo raia wa Russia wanapaswa kujiepusha kutembelea nchi hizo katika kipindi hicho.

Mashambulizi na mauaji ya kiholela ni jambo la kawaida katika nchi za Ulaya na hasa Marekani

 

Katika miezi ya hivi karibuni kumetokea mashambulizi mengi ya kigaidi katika nchi za Ulaya na Marekani na kupelekea makumi ya watu kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Mashambulizi mengi yamefanywa na wafuasi wa genge la kigaidi la ISIS (Daesh) na vile vile kumekuwa kukitokea mashambulizi ya kila siku ya kuuliwa watu kwa makundi huko nchini Marekani.

Wimbi la mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Marekani na Ulaya limeenea katika hali ambayo miaka ya hivi karibuni nchi hizo zilizidisha uadui wao kwa nchi za Kiislamu ikiwemo Syria kwa kuanzisha na kuyatia nguvu magenge ya kigaidi kama vile Daesh na kuyatuma katika nchi kama Syria na Iraq kwenda kufanya jinai za kutisha dhidi ya raia wa nchi hizo.