Mji wa London washuhudia maandamano ya kutaka kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37587-mji_wa_london_washuhudia_maandamano_ya_kutaka_kuachiliwa_huru_sheikh_zakzaky
Maelfu ya wakazi wa mji mkuu wa Uingereza London, wameandamana wakitaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 14, 2017 03:22 UTC
  • Mji wa London washuhudia maandamano ya kutaka kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky

Maelfu ya wakazi wa mji mkuu wa Uingereza London, wameandamana wakitaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamekusanyika mbele ya jengo la ubalozi wa Nigeria mjini London na kulalamikia kuendelea kushikiliwa kinyume cha Sheria Sherikh Ibrahim Zakkzaky.

Maandamano hayo ambayo yamefanyika kwa mnasaba wa kutimia miaka miwili ya kuendelea kushikiliwa kinyume cha sheria Sheikh Ibrahim Zakzaky yameshuhudia nara za kulaani vitendo vya ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Nigeria.

Waandamanaji hao wameitaka serikali ya Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria kumuachilia huru mwanaharakati huyo wa Kiislamu na kutaka kukomeshwa vitendo vya ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Sheikh Ibrahim Zakzaky Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Aidha waandamanaji hao wamesisitiza kwamba, Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria anashikiliwa kinyume cha sheria na vyombo vya usalama vya nchi hiyo, hivyo anapaswa kuachiliwa huruu mara moja.

Itakumbukwa kuwa, Sheikh Ibrahim Zakzaky alitiwa nguvuni na jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 baada ya kuvamia makazi yake katika mji wa Zaria jimboni Kaduna na kufanya mauaji ya umati dhidi ya Waislamu. Hata hivyo licha ya mahakama kutoa hukumu ya kutaka kuachiwa huru mwanazuoni huyo, bado vyombo vya usalama vya Nigeria vinaendelea kumshikilia katika korokoro isiyojulikana huku ripoti zikifichua kwamba hali yake ya kiafya ni mbaya.