Uchaguzi wa rais waanza leo Russia, Putin anatazamiwa kushinda
Uchaguzi wa rais wa Russia umenza mapema leo kote nchini humo huku Rais wa sasa wa nchi hiyo, Vladimir Putin akitazamiwa kupata ushindi mkubwa dhidi ya wapiznani wake.
Uchaguzi huo umeanza rasmi mapema leo katika maeneo ya mashariki kabisa mwa Russia ya Petropavlovsk na Kamchatsky na utaendelea kwa masaa 22 hadi katika jimbo la magharibi mwa nchi hiyo la Kaliningrad.
Wagombe saba wanachuana katika uchaguzi huo wa rais wa Russia na mpinzani mkubwa zaidi wa Rais Vladimir Putin anatajwa kuwa ni Pavel Grudinin anayebeba bendera ya Chama cha Kikomunisti.
Uchunguzi wa maoni unaonesha kuwa, Putin anaungwa mkono na karibu asilimia 70 wapiga kura wa Russia ikiwa ni mara kumi zaidi ya mpinzani wake wa karibu. Wapiga kura wengi wanamtambua Vladimir Putin, aliyekuwa jasusi wa shirika la upelelezi la Russia KGB, kuwa anatetea vyema maslahi ya nchi hiyo kote dunia licha ya msuguano wa mara kwa mara na nchi za Magharibi.
Rais mpya wa Russia ataiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 6