Uchunguzi: Wamarekani weusi wanauliwa na polisi kwa makusudi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i4624-uchunguzi_wamarekani_weusi_wanauliwa_na_polisi_kwa_makusudi
Matokeo ya uchunguzi mpya uliofanyika nchini Marekani yanaonesha kuwa vitendo vya polisi ya nchi hiyo vya kuwaua kwa kuwapiga risasi Wamarekani wenye asili ya Afrika tena wasio na silaha, vinaongezeka.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 08, 2016 03:28 UTC
  • Uchunguzi: Wamarekani weusi wanauliwa na polisi kwa makusudi

Matokeo ya uchunguzi mpya uliofanyika nchini Marekani yanaonesha kuwa vitendo vya polisi ya nchi hiyo vya kuwaua kwa kuwapiga risasi Wamarekani wenye asili ya Afrika tena wasio na silaha, vinaongezeka.

Ripoti iliyochapishwa jana na gazeti la Washington Post imesema matokeo ya uchunguzi wa wahakiki wa Chuo Kikuu cha Louisville na Chuo Kikuu cha North Carolina yanaonesha kuwa, katika mwaka uliopita wa 2015 polisi wa Marekani waliwalenga sana kwa risasi Wamarekani weusi ambao hawakuwa na silaha. Ripoti hiyo imesema polisi waliohusika na mauaji ya Wamarekani hao wenye asili ya Afrika walidai kuwa walihisi wanatishiwa na raia hao ambao hawakuwa na silaha!

Ripoti hiyo inatazamiwa kukabidhiwa kwa wanachama wa Jumuiya ya Vituo vya Polisi katika miji muhimu ya Marekani.

Polisi ya Marekani inalaumiwa kwa kuwalenga kwa risasi raia wenye asili ya Afrika kutokana na sababu za kibaguzi.