Feb 05, 2022 14:16 UTC
  • Wanaharakati wa haki za binadamu Marekani waandamana baada ya kuachiwa polisi aliyeua kijana mweusi

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamefanya maandamano nchini Marekani kupinga hatua ya kuachiwa huru afisa wa polisi aliyemuua kijana mweusi.

Ripoti zinasema wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekusanyika katika eneo la Federal Square kwenye mji wa Chicago wakipinga kuawachiwa huru afisa wa zamani wa polisi, Jason Van Dyke, ambaye mwaka 2014 alimpiga risasi na kumuua kijana mweusi aliyekuwa na umri wa miaka 17, Laquan McDonald.

Afisa huyo wa polisi ya Marekani alidai mahakamani kuwa alidhani kwamba kijana huyo alikuwa na nia ya kumshambulia kwa kisu. Mahakama ilikataa madai ya Jason Van Dyke na kumtia hatiani. Van Dyke ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo kwa muda wa miaka 6 na nusu tu. 

Tangu mwaka wa 2013, kulingana na data ya Unyanyasaji wa Polisi wa Marekani (Mapping Police Violence), Wamarekani 1,100 wameuawa kila mwaka katika ukatili wa polisi.

Utafiti wa hivi majuzi wa Chuo Kikuu cha Washington ulibaini kwamba Wamarekani weusi wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi wa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi kuliko kundi lolote lingine katika jamii ya Marekani na kwamba uwezekano wa Mmarekani mweusi kuuawa na polisi ni mara 3.5 zaidi kuliko Wamarekani weupe.

Tags