Mbunge Mwislamu wa Kongresi ya Marekani: Trump ni mbaguzi wa rangi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50009-mbunge_mwislamu_wa_kongresi_ya_marekani_trump_ni_mbaguzi_wa_rangi
Mbunge mpya Mwislamu wa Kongresi ya Marekani amesema kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ni mbaguzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 07, 2018 04:05 UTC
  • Rashida Tlaib
    Rashida Tlaib

Mbunge mpya Mwislamu wa Kongresi ya Marekani amesema kuwa, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ni mbaguzi.

Rashida Tlaib aliyeshinda katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Bunge la Marekani amesema kuwa, matamshi ya Donald Trump yanafichua sera zake za kibaguzi na kiongozi huyo anapaswa kuwajibishwa na kusailiwa kwa matamshi hayo. 

Mbunge huyo wa Marekani ameongeza kuwa, ujumbe unaotolewa mara kwa mara na Trump katika mtandao wa kijamii wa Twitter unawakanganya wanasiasa na wananchi wa Marekani.

Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akishambuliwa sana na wanasiasa na wananchi wa Marekani kutokana na sera zake za kibaguzi. Hivi karibuni pia mbunge Sheila Jackson-Lee wa chama cha Democratic katika jimbo la Texas alimkosoa vikali Trump baada ya kiongozi huyo kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya waandishi habari watatu wenye asilili ya Afrika. Vilevile Donald Trump amekosolewa sana kutokana na matamshi yake dhidi ya nyota wa mpira wa kikapu wa nchi hiyo, Lebron James.

Mwezi Agosti mwaka huu Trump alimshambulia nyota huyo wa ligi ya NBA akisema ni mtu asiye na akili na uelewa.