Wanaharakati wa kiraia mjini Vienna wafanya maandamano kupinga uzayuni
(last modified Sun, 02 Jun 2019 07:50:53 GMT )
Jun 02, 2019 07:50 UTC
  • Wanaharakati wa kiraia mjini Vienna wafanya maandamano kupinga uzayuni

Mamia ya Waislamu na wanaharakati wa makundi ya kiraia nchini Austria, wamefanya maandamano mjini Vienna, wakipinga jinai na ukatili wa utazala haramu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina.

Washiriki wa maandamano hayo wameunga mkono nchi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Pakistan, Afghanistan na Uturuki ambazo ni wabeba bendera na picha za mashahidi wa muqawama wa matukufu ya taifa la Palestina. Maandamano hayo ya kulaani utawala wa Kizayuni yamejiri katika hali ambayo Ijumaa iliyopita, mamilioni ya Waislamu na watetezi wa haki za binaadamu walishiriki maandamano makubwa ya Siku ya Kimataifa ya Quds duniani kwa ajili ya kuwaunga mkono raia wa Palestina na kusisitiza azma ya kukombolewa ardhi za taifa hilo linalokaliwa kwa mabavu. Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na kupitia ubunifu wa Imam Khomeini (MA), Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, inatambuliwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds.

Miaka yote Siku ya Kimataifa ya Quds huadhimishwa kona mbalimbali za dunia

Ambapo Waislamu kote duniani huonyesha hasira zao mbele ya siasa za kibaguzi na za kupenda kujitanua za utawala katili wa Israel. Katika hatua nyingine utawala huo wa Kizayuni umeripotiwa kuuza misaada ya kibinadamu inayotolewa na nchi za Ulaya kwa ajili ya Wapalestina. Kanali ya televisheni ya Al-Alam imeripoti kwamba utawala huo wa kibaguzi umekuwa ukiuza kwa namna ya mnada misaada inayotolewa na nchi za Ulaya kwa ajili ya ujenzi wa shule eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Hata hivyo utawala huo katili umedai kwamba misaada hiyo ilikuwa haina kibali na hivyo kuamua kuipiga mnada.