Iran na Uturuki kuanzisha mfumo wao wa kifedha ili kuimarisha biashara
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53868-iran_na_uturuki_kuanzisha_mfumo_wao_wa_kifedha_ili_kuimarisha_biashara
Serikali za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki zimekusudia kuanzisha mfumo wao mpya wa kifedha kwa ajili ya kuimarisha biashara kati ya pande mbili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 02, 2019 03:33 UTC
  • Iran na Uturuki kuanzisha mfumo wao wa kifedha ili kuimarisha biashara

Serikali za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki zimekusudia kuanzisha mfumo wao mpya wa kifedha kwa ajili ya kuimarisha biashara kati ya pande mbili.

Mohammad Farazmand, balozi wa Iran nchini Uturuki amesema kuwa, kuanzishwa mfumo huo wa kifedha kati ya Tehran na Ankara utasaidia kuimarisha biashara kati ya pande mbili katika kukabiliana na vikwazo vya upande mmoja vya Marekani. Akibainisha kwamba Iran na Uturuki zimekusudia kuanzisha benki ya pamoja amebainisha kwamba nchi mbili zinaweza kuanzisha mfumo wa mabadilishano katika uwanja wa biashara kwa kutumia sarafu zao za kitaifa. 

Mohammad Farazmand, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uturuki

Mohammad Farazmand, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uturuki amesisitiza kwamba kustawishwa biashara kati ya pande mbili, ni haki ya nchi zote. Aidha ameashiria ununuzi wa Uturuki wa gesi ya Iran na kuongeza kwamba suala hilo linahitajia mfumo mpya ambao umeanza kutumika kwa kiwango fulani. Viongozi wa Iran na Uturuki wana uhusiano wa kibiashara wenye thamani ya dola bilioni 30.