Viongozi wa Venezuela, Cuba wajadili njia za kukabiliana na Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53993-viongozi_wa_venezuela_cuba_wajadili_njia_za_kukabiliana_na_marekani
Makamo wa Rais wa chama tawala cha Venezuela Diosdado Cabello amekutana na kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba, Raul Castro kwa lengo la kujadili njia za kukabiliana na uhasama wa Marekani dhidi ya nchi zao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 08, 2019 11:51 UTC
  • Viongozi wa Venezuela, Cuba wajadili njia za kukabiliana na Marekani

Makamo wa Rais wa chama tawala cha Venezuela Diosdado Cabello amekutana na kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha Cuba, Raul Castro kwa lengo la kujadili njia za kukabiliana na uhasama wa Marekani dhidi ya nchi zao.

Cabello, ambaye ni kiongozi wa ngazi za juu katika serikali ya Rais Nicolas Maduro wa Venezuela, aliwasili Havana nchini Cuba Ijumaa na kusema kuna haja ya kuwepo umoja baina ya nchi hizo mbili katika kukabiliana na adui wa pamoja.

Naye Castro amenukuliwa akisema Cuba inawaunga mkono kikamilifu watu wa Venezuela na serikali yao katika mapambano dhidi ya Marekani.

Ikumbukwe kuwa, baada ya kushindwa katika uchaguzi wa rais, kinara wa upinzani Venezuela Juan Guaido alijitangaza kuwa rais wa muda hapo tarehe 23 Januari mwaka huu kupitia uungaji mkono kamili wa Marekani.

Rais Trump wa Marekani na kinara wa upizani Venezuela Juan Guaido

Hata hivyo licha ya njama hizo za kutaka kumuondoa madarakani Rais Maduro, jeshi na wananchi pamoja na nchi kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, China, Afrika Kusini na mataifa mengi ya dunia yameendelea kusisitiza ulazima wa kuheshimiwa haki ya kujitawala nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Katika upande mwingine, hivi karibuni Rais Donald Trump alinukuliwa akitishia kwamba, atachochea mapinduzi ya kijeshi nchini Cuba na kuiwekea Havana vikwazo vikali kabisa endapo nchi hiyo haitaondoa vikosi vyake vya jeshi huko Venezuela, vitisho ambayo vimepuuzwa na viongozi wa nchi hiyo.