UN: Magaidi elfu 30 wa kundi la Daesh wangali hai
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55085-un_magaidi_elfu_30_wa_kundi_la_daesh_wangali_hai
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh elfu 30 wangali hai.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 30, 2019 11:04 UTC
  • UN: Magaidi elfu 30 wa kundi la Daesh  wangali hai

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh elfu 30 wangali hai.

Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti iliyoitoa Jumatatu wiki hii ukiutaja mji wa Idlib nchini Syria kuwa moja ya maficho makubwa zaidi ya magaidi wa nchi ajinabi, na kukadiria kwamba kuna uwezekano karibu magaidi elfu 30 wa kundi la Daesh wangali hai. Umoja wa Mataifa umekumbusha katika ripoti yake hiyo kuwa makundi ya kigaidi ya Daesh na al Qaida yanashindana kuwa na nguvu katika maeneo mengi.  

Umoja wa Mataifa umeripoti pia kuhusu vyanzo vya fedha vya kundi la Daesh na kueleza kuwa: Zipo tetesi kwamba kundi hilo la kigaidi bado lina utajiri wa kiasi cha dola milioni 50 hadi 300 hata hivyo kundi hilo halina fedha za kutosha ili kutekeleza operesheni zake. 

Julian King Kamishna wa Masuala ya Usalama wa Umoja wa Ulaya Alhamisi iliyopita alisema katika kikao cha ukaguzi cha Bunge la Ulaya kwamba kwa mujibu wa makadirio kuhusu masuala ya kiusalama, magaidi wa Daesh wapatao 5,500 walielekea Iraq na Syria kupigana vita. Nchi za Magharibi ambazo hazikuacha kufanya juhudi zozote za kuwasaidia magaidi katika eneo la Asia Magharibi khususan huko Syria hivi sasa zina wasiwasi kuhusu kurejea nyumbani magaidi hao wa Ulaya na mashambulizi wanayoweza kutekeleza katika nchi hizo. 

Magaidi wa nchi za Ulaya wanachama wa Daesh katika hujuma zao nchini Iraq