Dec 07, 2019 02:47 UTC
  • FAO: Bei ya chakula duniani imepanda kuanzia mwezi Novemba

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa bei ya chakula duniani imepanda ndani ya mwezi uliopita wa Novemba.

Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema, bei ya chakula ndani ya mwezi huo ilipanda kwa asilimia 2.7 ikilinganishwa na mwezi wa kabla yake. Kwa mujibu wa shirika hilo, ongezeko kubwa la bei lilishuhudiwa kwenye nyama na mafuta ya nafaka. Aidha limeongeza kwamba tangu mwanzoni mwa mwaka huu kulikuwepo na mlingano wa viwango vya bei ambapo baada ya kushuka mtawalia kwa bei katika kipindi cha miezi mitatu, baadaye iliongezeka tena.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema kuwa hadi sasa kiwango cha bei ya chakula kilichoainishwa na shirika hilo mwaka huu kimepanda kwa asilimia 9.5 kulinganisha na kiwango kilichoainishwa mwaka uliopita. Hayo yanajiri wakati hapo kabla shirika hilo lilitangaza kuwa, kilimo cha kutumia mbolea za kemikali kimechangia kwa asilimia kubwa kuongezeka kwa ukosefu wa chakula katika nchi zinazoendelea hali inayolazimu wakulima kuanza kujifunza kilimo hai ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hayo yalisemwa na Fred Cafero mwakilishi mkazi wa FAO nchini Tanzania ambapo alibainisha kwamba kilimo hai kinaweza kuongeza tija kwa mkulima.

Tags