Sanders asusia mkutano wa loby ya Wayahudi wa Marekani, AIPAC
-
Bernie Sanders
Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani anayeongoza katika mbio za kuwakilisha chama cha Democratic katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo ametangaza kuwa hatashiriki katika mkutano wa kila mwaka wa lobi na kundi la mashinikizo la Wayahudi wa Marekani, "AIPAC.
Bernie Sanders amesema kuwa ajenda ya AIPAC kwa ajili ya maafisa wa Marekani imejaa chuki na inapinga haki za kimsingi za taifa la Palestina na inatia wasiwasi.
Bernie Sanders amesisitiza kuwa hatashirkii katika mkutano wa kila mwaka wa AIPAC ambao umepangwa kufanyika wiki ijayo mjini Washington.
Wakati huo huo kundi hilo la mashinikizo la Wazayuni nchini Marekani la AIPAC limetangaza kuwa, haliridhishwi na hatua ya Bernie Sanders ya kususia mkutano wake. AIPAC imedai kuwa, watu wanaoshiriki katika mkutano huo wanataka kuimarisha zaidi uhusiano wa Marekani na Israel.
Awali Bernie Sanders alimtaja Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu kuwa ni mbaguzi na kuitaka Washington ibadili siasa na misimamo yake kuhusiana na Wapalestina.
Bernie Sanders mbaye yeye mwenyewe ni Myahudi amesema, iwapo hatutaamilia kwa heshima na Wapalestina haitawezekana kupatikana amani katika eneo la Mashariki ya Kati.