Korea Kaskazini yafanya jaribio jengine la makombora
(last modified Mon, 02 Mar 2020 07:32:09 GMT )
Mar 02, 2020 07:32 UTC
  • Korea Kaskazini yafanya jaribio jengine la makombora

Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imetangaza kuwa Korea Kaskazini imefanya jairbio jengine la makombora.

Vyombo vya habari kutoka Seoul vimeinukuu wizara ya ulinzi ya nchi hiyo ikitangaza kuwa, makombora hayo mawili yamefyatuliwa mapema leo katika mji wa Korea Kaskazini wa Wonsan kuelekea baharini.

Tarehe mosi Januari, Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitangaza kuwa, miradi ya nyuklia na majaribio ya makombora ya nchi yake yataanza tena endapo mazungumzo ya nchi hiyo na Marekani hayatoanza tena.

Mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini hivi sasa yameingia kwenye mkwamo baada ya kuvunjika mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliyofanyika Hanoi, Vietnam mnamo mwezi Februari mwaka 2019.

Trump (kushoto) na Kim walipokutana kwa mara kwanza nchini Singapore

Kwa mara ya kwanza, Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walikutana na kufanya mazungumzo Juni 12, 2018 nchini Singapore kabla ya kukutana tena mjini Hanoi, Vietnam kwa mazungumzo rasmi Februari 28 na 29, 2019 ambayo yalivunjika baada ya muda mfup kutokana na pande mbili kushindwa kufikia maelewano.../

Tags