Uchumi wa Marekani wavunja rekodi, waporomoka kwa asilimia 32.9
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62534-uchumi_wa_marekani_wavunja_rekodi_waporomoka_kwa_asilimia_32.9
Uchumi wa Marekani uliporomoka kwa asilimia 32.9 katika robo ya pili ya mwaka huu, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1947.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 31, 2020 21:55 UTC
  • Uchumi wa Marekani wavunja rekodi, waporomoka kwa asilimia 32.9

Uchumi wa Marekani uliporomoka kwa asilimia 32.9 katika robo ya pili ya mwaka huu, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 1947.

Wizara ya Biashara ya Marekani imetangaza makadirio yake ya kwanza kuhusu ukuaji wa uchumi, ikisema kuwa kutokana na kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi na matumizi kunakosababishwa na janga la COVID-19 au corona, Pato la Ndani la Marekani liliporomoka kwa asilimia 32.9 katika robo ya pili ya mwaka huu

Takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi hicho, matumizi binafsi yanayochangia asilimia 70 ya uchumi wa Marekani, yalipungua kwa asilimia 34.6 kutokana na watu kusalia majumbani. Matumizi ya huduma yaliyoathiriwa vibaya kutokana na mlipuko wa COVID-19 yalishuka kwa asilimia 43.5.

Rais Trump

Ili kuzuia kuenea kwa virusi vya COVID-19, Marekani ilianza kutekeleza amri ya kukaa nyumbani na kufunga sehemu zisizo na ulazima wa kufunguliwa kuanzia mwezi Machi, na kusababisha mporomoko mkubwa zaidi wa uchumi ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya hivi karibuni ya nchi hiyo.