Umoja wa Mataifa umetaka kuachiwa huru mwanaharakati kike wa Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65457
Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo mwanaharakati wa kike wa nchi hiyo anayejulikana kwa jina la Loujain Alhathloul.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 29, 2020 03:01 UTC
  • Umoja wa Mataifa umetaka kuachiwa huru  mwanaharakati kike wa Saudia

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetaka kuachiwa huru haraka iwezekanavyo mwanaharakati wa kike wa nchi hiyo anayejulikana kwa jina la Loujain Alhathloul.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa aidha imelaani hukumu ya kifungo cha jela aliyokatiwa mwanaharakati huyo. Katika hukumu  isiyo ya uadilifu, Mahakama ya Jinai ya Riyadh jana Jumatatu ilimhukumu kifungo cha miaka 5 na miezi 6 jela Loujain Alhathloul, mwanahakati wa kike wa nchini humo. 

Mahakama ya Uhalifu ya Saudi Arabia awali ilitoa hukumu na kuwasilisha faili la kesi ya bi Alhathloul katika mahakama ya ugaidi. Wakati huo huo Aliya Alhathloul dada wa mwanaharakati huyo wa kike wa Saudi Arabia amesema kuwa: ndugu yake amekuwa chini ya mashinikizo makali ya kisaikolojia ya kumlazimisha akiri makosa; na kwamba hali yake ya kimwili si nzuri.  

Free Loujain  

Bi Loujain ambaye amekuwa korokoroni kuanzia mwezi Mei mwaka 2018; tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu alifanya mgomo wa kula akilalamikia kunyimwa fursa ya kuwasiliana na familia yake. 

Mwanaharakati huyo wa Saudia zaidi alikuwa akipigania wanawake nchini humo waruhusiwe kuendesha magari lakini Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi hiyo alimtuhumu Loujain kuwa anadhuru maslahi ya nchi hiyo.