Uchunguzi wa maoni kimataifa: Marekani ni tishio kuu zaidi kwa demokrasia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i69820-uchunguzi_wa_maoni_kimataifa_marekani_ni_tishio_kuu_zaidi_kwa_demokrasia
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika katika nchi 53 duniani yameonyesha kuwa, Marekani ndio tishio kubwa zaidi kwa demokrasia.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
May 05, 2021 22:39 UTC
  • Uchunguzi wa maoni kimataifa: Marekani ni tishio kuu zaidi kwa demokrasia

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanyika katika nchi 53 duniani yameonyesha kuwa, Marekani ndio tishio kubwa zaidi kwa demokrasia.

Gazeti la The Guardian la Uingereza limeripoti kuwa, uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Muungano wa Wanademokrasia unaonyesha kuwa asilimia 65 washiriki katika uchunguzi huo kwenye nchi zenye demokrasia ndogo, wanaridhishwa na jinsi serikali zao zilivyopambana na maambukizi ya virusi vya corona. 

Matokeo hayo yanasema kuwa, asilimia 51 tu ya washiriki katika uchunguzi huo kwenye nchi zenye demokrasia kubwa zaidi ndio wanaoridhishwa na jinsi serikali za nchi zao zilivyopambana na corona. Kiwango hicho katika nchi za Asia ni asilimia 76. 

Wakati huo huo matokeo ya uchunguzi huo wa maoni wa kimataifa yanaonyesha kuwa, asilimia 44 ya washiriki katika uchunguzi huo wanaamini kuwa, Marekani ni tishio kubwa zaidi kwa demokrasia katika nchi zao. Hii ni licha ya Marekani kudai kuwa kinara wa demokrasia duniani. 

Kiwango hicho kuhusiana na China ni asilimia 38 na wengine 28 tu ndio waliosema kuwa Russia ni tishio kwa demokrasia.

Vilevile asilimia 64 ya watu katika nchi mbalimbali za dunia wanasema ukosefu wa usawa wa kiuchumi ni tishio kwa demokrasia. 

Awali Umoja wa Mataifa ulikuwa umetahadharisha kuwa, demokrasia inaendelea kudhoofishwa nchini Marekani na umetoa maagizo kuhusu jinsi ya kung'oa mizizi ya umaskini nchini humo. 

Matatizo makubwa na yanayozidi kuongezeka ya kiuchumi ambayo yamesababishwa na wimbi la maambukizi ya corona pia yamezidisha hali ya kutoridhishwa Wamarekani na utendji wa serikali ya nchi yao.