Merkel aitaka jamii ya kimataifa kuzungumza na Taliban
https://parstoday.ir/sw/news/world-i73926-merkel_aitaka_jamii_ya_kimataifa_kuzungumza_na_taliban
Kinyume kabisa na msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu kundi la wanamgambo wa Taliban la Afghanistan, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameitolea mwito jamii ya kimataifa kufanya mazungumzo na kundi hilo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 26, 2021 03:44 UTC
  • Merkel aitaka jamii ya kimataifa kuzungumza na Taliban

Kinyume kabisa na msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu kundi la wanamgambo wa Taliban la Afghanistan, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameitolea mwito jamii ya kimataifa kufanya mazungumzo na kundi hilo.

Akizungumza bungeni, Angela Merkel ameitaka jamii ya kimataifa kuzungumza na kundi la Taliban na kudai kuwa Berlin itaendelea kuwasaidia Waafghani baada ya wanajeshi wa nchi hiyo kuondoka Afghanistan.

Hii ni katika hali ambayo, Ursula Von der Leyen Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya na Josep Borrell Mkuu wa Sera za Nje wa umoja huo hivi karibuni walisisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya hauna nia ya kulitambua rasmi kundi la Taliban licha ya umoja huo kuendelea kuwasiliana na kundi hilo. 

Wanamgambo wa Taliban 

Jumapili tarehe 15 mwezi huu serikali ya Rais Ashraf Ghani ilisambaratika na kiongozi huyo kuikimbia nchi baada ya Taliban kuingia Kabul mji mkuu wa Afghanistan. Wachambuzi wa mambo wanasema, hatua ya wanamgambo wa Taliban kuudhibiti mji wa Kabul imehitimisha uvamizi wa miaka 20 wa Marekani na nchi nyingine za Magharibi kwa kisingizio cha kuijenga upya Afghanistan.  

Aghalabu ya viongozi na wananchi wa Afghanistan wanaamini kuwa, hali ya sasa ya nchi hiyo ni matokeo ya siasa zilizofeli za Marekani nchini humo.