UN yatahadharisha: Bosnia inakabiliwa na hatari ya vita na kugawanyika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i76478-un_yatahadharisha_bosnia_inakabiliwa_na_hatari_ya_vita_na_kugawanyika
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Bosnia Hezregovina ametahadharisha kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hatari ya vita na kugawanyika.
(last modified 2025-11-30T09:37:44+00:00 )
Nov 03, 2021 07:42 UTC
  • UN yatahadharisha: Bosnia inakabiliwa na hatari ya vita na kugawanyika

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Bosnia Hezregovina ametahadharisha kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hatari ya vita na kugawanyika.

Christian Schmidt ametahadharisha kuwa, Bosnia Herzegovina imo katika hatari ya kugawanyika, na kuna uwezekano wa kutumbukia tena katika vita vya ndani kama ile ya muongo wa 1990. 

Katika ripoti yake iliyowasilishwa Umoja wa Mataifa, Christian Schmidt amesema kuwa, iwapo wale Waserbia wanaotaka kujitenga watatekeleza vitisho vyao vya kuunda tena kikosi cha jeshi na kuligawa jeshi la sasa la taifa, kutahitajika askari zaidi wa kimataifa wa kilinda amani ili kuzuia vita vipya nchini Bosnia.

Kwa sasa kikosi cha askari wa Ulaya maarufu kwa kifupi kama Eufor ambacho kina wanajeshi 700 ndicho kinacholinda amani huko Bosnia Herzegovina.

Vita vya Bosnia vya mwaka 1992 hadi 1995 vilisababisha mauaji ya watu laki moja na wengine milionii bili alilazimika kuwa wakimbizi. 

Maelfu ya Waislamu waliuawa katika vita vya Bosnia Herzegovina

Waserbia wa Bosnia pia walifanya jinai na mauuaji ya kutisha katika vita hivyo yakiwemo mauaji ya kimbari ya maelfu ya Waislamu wa mji wa Srebrenica.