UNEA yaidhinisha maazimio 25 ya kuimarisha maendeleo endelevu
Mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira UNEA2 umepasisha maazimio 25 yanayolenga kuchochea zaidi maendeleo endelevu yasiyochafua mazingira.
Katika mkutano wa siku tano uliofanyika mjini Nairobi Kenya, mawaziri, watunga sera na wakuu wa viwanda kutoka nchi 174 walipasisha maazimio hayo ya kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa, uchafuzi wa bahari, kemikali na uhalifu dhidi ya wanyama pori.
Mkurungezi wa Shirika la kulinda Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, Achim Steiner amesema, wanatarajia kuchukuliwa hatua muhimu za kujitlolea kwwa viwango vya kitaifa ili kuendeleza ajenda ya mwaka 2030 ya kuhakikisha ufanikishaji wa mustakabali mzuri kwa watu na sayari ya dunia.
Maudhui ya mkutano huo wa UNEA yalikuwa ni kuhusu mazingira na maendeleo endelevu yaliyoidhinishwa na nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka jana.
Wajumbe pia walijadili mikakati ya kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya mabadiliko ya hali ya hewa yalioidhinishwa mwezi Disemba mwaka jana mjini Paris Ufaransa.