Mar 17, 2022 08:51 UTC
  • Vituo vya Kiislamu vya Russia vyalaani mashambulizi ya kipropaganda ya Magharibi dhidi ya nchi hiyo

Vituo vya Kiislamu vya Russia vimelaani propaganda za chuki za nchi za Magharibi dhidi ya Moscow na ubaguzi dhidi ya raia wa Russia.

Wawakilishi wa taasisi na mashirika ya Kiislamu ya Russia wametoa taarifa ya kuunga mkono operesheni ya kijeshi ya nchi hiyo nchini Ukraine, wakilaani propaganda za uadui za nchi za Magharibi dhidi ya Moscow na ubaguzi unaofanywa dhidi ya raia wa Russia.

Taarifa hiyo imesema, matukio ya hivi sasa yanathibitisha kwamba nguvu ya Russia imo katika kuwepo kaumu tofauti na umoja katika kulinda nchi.

Taarifa hiyo imewapongeza wanajeshi Waislamu katika jeshi la Russia linalopigania amani, usalama na ustawi wa watu wa Donbas. Imeashiria kashfa na jinai za nchi za Magharibi huko Iraq, Libya na Syria, na kusema: Kukaribia kwa nchi za Magharibi katika mipaka ya Russia ni tishio la moja kwa moja la kijeshi na hakuna budi isipokuwa kuilinda nchi ili kukabiliana na suala hilo. 

Russia inaendelea kuandamwa na vikwazo na mashinikizo ya kila upande ya Marekani na washirika wake wa kutokana na uungaji mkono wake kwa Warusi wa Mashariki mwa Ukraine na kutambua rasmi uhuru na kujitawala maeneo ya Donetsk na Luhansk.

Tags