Wazee maskini wa Canada wanafadhilisha kifo kuliko uhai
Mwandishi wa habari wa Marekani anayeishi Amerika ya Kusini ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akisimulia hali ya wazee maskini na walemavu nchini Canada na kuandika kuwa, mfumo wa kibepari ni wa kikatili na kwamba nchi hiyo inawaua watu maskini.
Ben Norton, mwandishi wa Marekani anayeishi Amerika ya Kusini, amesema pia kwamba nchini Canada, wazee maskini wenye ulemavu wanafadhilisha wajiuewe kwa msaada wa daktari kwa sababu hawana uwezo wa kulipa kodi ya pango na kawaida hukosa makazi.

Canada ni miongoni mwa nchi zinazojigamba kuwa mojawapo ya vinara wakuu wa haki za binadamu, na katika vikao vya kimataifa kama vile Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, daima imekuwa ikielekeza mishale yake mikali ya ukosoaji kwa baadhi ya nchi zinazopinga kutawaliwa na kudhibitiwa na nchi za Magharibi.
Hata hivyo, rekodi ya haki za binadamu ya nchi hiyo ina madoa mengi za giza, mojawapo ya muhimu zaidi ni unyanyasaji dhidi ya wenyeji na wakazi asilia wa Canada, unyanyasa wa aina mbalimbali, ubaguzi na mashinikizo yanayofanywa dhidi ya jamii hiyo.