Mar 13, 2023 02:36 UTC
  • Shakhsia zaidi ya 200 duniani wataka kukabiliana na ubaguzi katika ugavi wa chanjo ya corona

Zaidi ya shakhsia 200 duniani wamewatolea wito viongozi wa dunia kuchukua hatua ili kukabiliana na ubaguzi katika ugavi wa chanjo za kujikinga na corona.

Shakhsia hao 200 duniani wamekosoa kukosekana usawa katika ugavi wa chanjo za corona na namna nchi zilizoendelea zilivyosababisha kupoteza maisha zaidi ya watu milioni moja katika nchi maskini. Hayo yamebainishwa katika maadhimisho ya kutumia mwaka wa tatu tangu dunia ikumbwe na janga hatari la corona.  

Watu hao mashuhuri zaidi ya 200 kutoka pembe mbalimbali duniani wamesaini taarifa na kukosoa vizuizi na vigingi vilivyoziathiri nchi zilizo na pato la chini na ya wastani katika kupata chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Uviko-19 pale ulipoeenea kwa mara ya kwanza duniani. 

Wameeleza kuwa, vifo vya zaidi ya watu milioni moja vingeweza kuzuiliwa mwaka 2021 kama chanjo za corona zingegawiwa kwa uadilifu duniani. 

Janga la corona lilivyoangamiza mamilioni ya watu duniani 

Shakhsia hao aidha wamelaani kitendo cha makampuni ya kutengeneza dawa cha kuzidisha maradufu faida zao kupitia kuziuzia chanjo nchi tajiri badala ya kugawa kwa uadilifu chanjo hizo na kutoa huduma za tiba kwa mujibu wa mahitaji sahihi.  

Tags