Apr 17, 2023 06:30 UTC
  • Waislamu nchini Canada waendelea kukabiliwa na vitendo vya ubaguzi

Vitendo vya ubaguzi dhidi ya jamii ya Waislamu nchini Canada vimeendelea kushuhudiwa licha ya miito mbalimbali ya kukomesha ubaguzi huo.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, akthari ya Waislamu nchini Canada wamekuwa wakibaguliwa katika maeneo yao ya kazi na kwamba, ni wahanga wa vitendo vya ubaguzi katika nchi hiyo.

Taasisi ya Misaada ya Islamic Relief imesema katika ripoti yake mpya baada ya uchunguzi kwamba, zaidi ya theluthi mbili ya Waislamu wa Canada wamekuwa wakibaguliwa au kukabiliana na vitendo na miamala ya kibaguzi wakiwa katika maeneo yao ya kazi.

Ripoti ya Taasisi ya Misaada ya Islamic Relief imeeleza kuweko aina mbili za ubaguzi ambazo ni ubaguzi rasmi na usio rasmi  na kwamba, ubaguzi rasmi ni ule unaoshuhudiwa katika idara na maeneo ya kazi.

Waislamu wamekuwa wakiandamwa na vitendo vya ubaguzi barani Ulaya

 

Katika aina hii ya ubaguzi, Waislamu hawafanyiwi uadilifu na  hata hubaguliwa katika masuala kama ya mishahara, kupandishwa vyeo na kadhalika.

Aidha kwa mujibu wa ripoti hiyo, ubaguuzi usio rasmi dhidi ya Waislamu ni ule wanaofanyiwa na wafanyakazi wenzao na hata wateja.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, walimu wote wa kike Waislamu wanaovaa Hijabu katika jimbo la Quebec nchini Canada wamekuwa wakibaguliwa na wanakosa fursa za kazi kutokana na sheria ya kibaguzi ya kupiga marufuku vazi la hijabu.

Tags