Rais wa Russia: Tunatoa kipaumbele katika kupanua jeshi la wanamaji
Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa suala la kustafidi na vikosi vya wanamaji ndio kipaumbele kikuu katika operesheni maalum za kijeshi zinazotekelezwa na Russia huko Ukraine, na kwamba kuongezwa idadi ya vikosi hivyo ni kati ya vipaumbele vingine vya Moscow.
Rais Vladimir Putin wa Russia jana alikutana na kufanya mazungumzo na Sergei Shoigu Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo ambapo alibainisha kuwa, kipaumbele cha Russia ni kustafidi na vikosi vya jeshi la wanamaji na kwamba, vikosi hivyo kimsingi vinatumiwa katika operesheni maalum za kijeshi za nchi hiyo huko Ukraine na katika kila jambo linalohusiana na kuwalinda raia katika mkoa wa Donbas na mikoa mingine mpya.
Rais Putin amemhutubu Sergei Shoigu akisema:" pamoja na hayo, lengo la kupanuliwa vikosi vya jeshi la wanamaji la Russia khususan katika Bahari ya Pacific, linasalia kuwa suala muhimu; na kwa sababu hii, naomba muendelee na jukumu hili na pia mzingatie kupanua na kuimarisha hatua kama hizi katika oparesheni zingine za majini."
Ijumaa iliyopita Sergei Shoigu Waziri wa Ulinzi wa Russia alisema kuwa lengo kuu la kukagua meli za Russia katika Bahari ya Pacific, mpango ambao haukupangwa ni kuongeza uwezo wa vikosi vya jeshi la nchi hiyo wakukabiliana na kuzima hujuma yoyote ya adui inayoweza kutekelezwa kwa njia ya bahari.