Tuujue Uislamu (18)
Ni wasaa na wakati mwingine wapenzi wasikilizaji tunapokutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Tuujue Uislamu. Katika vipindi kadhaa vilivyotangulia, tulijaribu kuonyesha madhihiirisho ya nguvu na mipango ya Mungu kwa kuangazia matukio mbalimbali katika ulimwengu wa uumbaji, kwa sababu hakuna sababu ya wazi zaidi ya kuthibitisha uwezo wa Mungu usio na kikomo kuliko kujifunza na kuzama katika matukio ya ulimwengu.
Katika kipindi chetu cha leo ambacho ni sehemu ya 18 ya mfululizo huu tutatoa muhtasari wa yaliyopita. Kuweni nami hadi mwisho wa kipindi hiki.
Tunapotazama uumbaji wa Mungu, tunajiona tuko mbele ya nguvu kubwa isiyo na kikomo na isiyoweza kufikiriwa kuwa na kikomo. Kutafakari katika ulimwengu wa ajabu wa asili na ulimwengu tata ndani ya mwanadamu ni uthibitisho wa wazi zaidi wa kuelewa uwezo ni kuangalia aliyevileta hivi. Mwenyezi Mungu hana mfano duniani na maneno hayawezi kueleza uwezo na adhama yake. Ulimwengu wa uumbaji ni mkusanyo wa maajabu, na tunapotazama maajabu haya, tunahisi ukuu na adhama ya Muumba na kile ambacho si katika yeye kwa uoni na mtazamo wetu kinaonekana kuwa ni kidogo na dhalili. Kwa bahati nzuri, hii leo, kwa kupiga hatua elimu na kupatikana maendeleo ya elimu na ugunduzi wa baadhi ya siri za ulimwengu, milango ya teolojia na kumtambua Mungu imefunguliwa kwa wanadamu kiasi kwamba, tunaweza kusema kwa ujasiri kabisa kwamba vitabu vya sayansi ya asili na mafundisho ya vitabu hivi yamejaa masomo ya kumtambua Mwenyezi Mungu.
Qur’ani Tukufu imetaja uumbaji wa ulimwengu na viumbe vyote kuwa ni dalili na ishara za Mwenyezi Mungu, na inawaita watu wanaotafuta ukweli wachunguze madhihirisho ya uumbaji na kuutafakari kwa makini ili wafahamu kuwepo kwa Muumba.
Watu wenye busara wanakubali kwamba, popote ambapo kuna nidhamu na uratibu, inaonyesha kuwepo kwa aliyeweka nidhamu na mpangilio huo. Kulingana na wao, kadiri mpangilio na nidhamu inavyokuwa tata na makini zaidi, ndivyo inavyoweka wazi na kudhihiri elimu na maarifa ya hali ya juu ya aliyeweka nidhamu na mpangilio huo. Kwa mfano, katika mfumo wa jua, jinsi sayari zinavyofanya harakati, jinsi zilivyo na umbali wao kutoka jua na dunia kwa namna fulani haya yanahusiana na hali ya maisha duniani. Mpangilio na nidhamu hii ni muhimu kwa kadiri kwamba, ikiwa kutatokea mparaganyiko katika mwendo wa kawaida wa sayari hizi kuzunguka jua, maisha duniani yatakuwa hatarini.
Mwenyezi Mungu anaashiria hilo katika Aya ya 54 ya Surat al-A'raf:
Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Aidha anasema katika Aya ya 79 katika Surat Nahl kwamba:
Je! Hawawaoni ndege walivyo wat'iifu katika anga la mbingu? Hapana mwenye kuwashika isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanao amini.
Katika aya nyingi, Qurani Tukufu inamtaka mwanadamu kuweka hai roho ya utambuzi na kutazama mambo kwa uhalisia wake. Kwani muono wa mbali humuonyesha mwanadamu njia ya haki na kumfungulia ukweli mmoja baada ya mwingine.
Qur'an inaufasiri ulimwengu wa ndani wa mwanadamu kuwa ni nafsi; chanzo cha kufikiri kwenye faida na kugundua ukweli na uhakika wake. Anasema katikak Aya ya 53 ya Surat Fussilat:
Sema: Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi ikawa ndio mmeyakataa, ni nani aliye potea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali?
Aina tofauti za wanyama huishi duniani, ambapo kila mmoja kati ya wanyama hawa ana jukumu maalumu na ushawishi katika ulimwengu wa asili. Kujua siri za ajabu za maisha ya wanyama hutuongoza kwenye nguvu na mpango wa Mwenyezoungu katika uumbaji.
Na hadi hapa wapenzi wasikilizaji ndio tunafiikia tamati ya kipindi chetu cha leo. Tukutane tena katika sehemu nyingine ya mfululizo huu.