May 12, 2017 21:57 UTC
  • Jumamosi, Mei 13, 2017

Leo ni Jumamosi tarehe 16 Shaaban 1438 Hijria sawa na tarehe 13 Mei mwaka 2017 Milaadia.

Siku kama ya leo miaka 826 iliyopita, alifariki dunia mjini Baghdad Ibn Dahhan, mwanafasihi na mshairi wa Kiarabu aliyekuwa na ulemavu wa macho. Ibn Dahhan alisoma na kujifunza elimu zote zilizokuwa zimeenea katika zama zake, ikiwemo Fiqhi, tafsiri, tiba, nujumu na kadhalika na alikuwa msomi wa kuzingatiwa mno. Alimu na msomi huyo alikuwa mtunzi stadi wa mashairi. Aidha Ibn Dahhan alikuwa amebobea katika lugha za kifarsi, Kituruki, Kirumi, Kihindi na Kiarmenia.***

Ibn Dahhan

Katika siku kama ya leo miaka 304 iliyopita, alizaliwa mjini Paris Alexis Cloude Clairaut mwanahesabati mashuhuri wa Ufaransa. Alikuwa na hamu kubwa na somo la hesabati ambapo akiwa na umri mdogo wa miaka 18 alifanikiwa kujiunga na Chuo cha Sayansi cha Ufaransa. Clairaut alipata umashuhuri mkubwa duniani kutokana na utafiti makini aliofanya katika nyanya tofauti za sayansi. Msomi huyo aliaga dunia mwaka 1765. ***

Alexis Cloude Clairaut

Miaka 264 iliyopita katika siku kama ya leo, alizaliwa Lazar Carnot mwanasiasa, jenerali wa jeshi na mwanahisabati mashuhuri wa Kifaransa. Carnot anahesabiwa kuwa, muasisi wa elimu ya jiometri mpya. Lazar Carnot alikuwa mhandisi na mwanastratejia wa kijeshi. Aidha alikuwa mmoja wa viongozi wenye taathira katika ushindi wa wanamapinduzi wa Ufaransa. Baada ya ushindi wa mapinduzi ya Ufaransa Carnot alifanikiwa kushika nyadhifa za juu.***

Lazar Carnot

Siku kama ya leo miaka 194 iliyopita, Amir Ahmad Minai mshairina mwandishi wa Kihindi alizaliwa. Alianza kutunga mashairi tangu akiwa na umri wa miaka 15. Mashairi ya malengo huyu wa India yalikuwa ya aina yake. Nathari zake kama yalivyokuwa mashairi zilikuwa za kawaida na aina ya kipekee. Ahmad Minai ametunga mashairi mengi yanayowasifia watu wa nyumba ya Bwana Mtume saw.***

Amir Ahmad Minai

 

Miaka 110 iliyopita katika siku kama ya leo,  alizaliwa Bi Daphne du Maurier mwandishi wa riwaya, wasifu na thamthiliya wa Kiingereza. Maurier alizaliwa katika familia ya wanasanaa na iliyokuwa pia na wanafasihi. Ni kutokana na kukulia katika mazingira kama hayo, ndipo Bi Daphne du Maurier akafanikiwa kukuza kipaji chake katika uwanja wa uandishi. Miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri ni Scapegoat na Rebecca. Mwandishi huyo aliaga dunia mwaka 1889. ***

Daphne du Maurier

Na miaka 38 iliyopita, kulingana na kalenda ya Hijria Shamsiya, mkataba wa kutoshtakiwa Wamarekani nchini Iran au Capitulation Accord ulifutwa nchini kufuatia mapambano mtawalia ya wananchi Waislamu wa Iran, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Kiislamu na kuasisiwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Kwa mujibu wa sheria za mkataba huo, raia wa Marekani aliyekuwa nchini Iran alikuwa na kinga kamili ya kisheria dhidi ya kufunguliwa mashtaka. Kwa kadiri kwamba hakuna taasisi au chombo chochote cha kisheria cha Iran kilichokuwa na mamlaka ya kumfungulia mashtaka na kumhukumu raia wa Marekani aliyekuweko Iran na kesi za raia hao wa Kimarekani zilipaswa kusikilizwa katika nchi yao. ***

Capitulation