Jul 03, 2017 08:54 UTC
  • Jumatatu 7 Julai, 2017

Leo ni Jumatatu tarehe 8 Mfunguo Mosi Shawwal 1438 Hijria mwafaka na tarehe 3 Julai mwaka 2017.

Siku kama ya leo miaka 29 iliyopita ndege ya abiria aina ya Airbus ya shirika la ndege la Iran iliyokuwa ikitoka Bandar Abbas, kusini mwa Iran na kuelekea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, ilishambuliwa kwa makombora mawili ya jeshi la Marekani kwenye maji ya Ghuba ya Uajemi. Manowari ya kijeshi ya Marekani USS Vincennes ilifyatua makombora hayo na kuua shahidi watu wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo. Shambulio hilo lilidhihirisha zaidi unyama wa serikali ya Marekani. Viongozi wa Marekani walizidisha ukatili wao pale walipomzawadia medali ya ushujaa nahodha wa meli hiyo kutokana na kitendo hicho kilichoonekana na serikali ya Washington kuwa eti ni cha kishujaa.

Ndege ya abiria ya Iran Air iliyotunguliwa na Marekani

Tarehe 12 Tir 1349 Hijria Shamsia, yaani miaka 47 iliyopita alifariki dunia Allamah Abdul Hussein Amini, faqihi mkubwa na mwandishi hodari na mashuhuri wa Kiislamu. Kitabu cha kwanza cha mwanazuoni huo alikipa jina la Shuhadaul Fadhila. Hata hivyo kitabu mashuhuri na kikubwa zaidi cha Allamah Amini ni kile cha "al Ghadiir Fil Kitabi Wassunah". Ndani ya kitabu hicho Allama Amini amekosoa na kuchunguza vitabu vikubwa na marejeo vya Kiislamu 150 akithibitisha wilaya na haki ya Imam Ali bin Abi Twalib ya kuwa Khalifa na Imam wa Waislamu baada tu ya Mtume Muhammad (saw). Mwanazuoni huyo alisafiri kwa taabu katika nchi nyingi kama India, Uturuki, Syria, Misri na Iraq kwa ajili ya kukusanya ushahidi mbalimbali wa kihistoria alioutumia katika kitabu hicho.

Allamah Abdul Hussein Amini

Siku kama ya leo miaka 94 iliyopita, Mawahabi wa Saudi Arabia walibomoa makaburi ya Ahlul Bait wa Mtume (s.a.w) ambayo yako Baqii, katika mji mtakatifu wa Madina. Baada ya Muhammad Ibn Saud kutawala tena maeneo ya Hijaz, likiwemo eneo la Madina, sheikh Abdullah bin Bulaihad aliyekuwa mkuu wa makadhi wa Kiwahabi, alitoa fatwa ya kuhalalisha kuharibiwa makaburi matukufu na ya kihistoria ya mjini Madina. Mawahabi walikusanya watu kwa nguvu na kuwalazimisha kwenda katika makaburi hayo ya Baqii na kuanza kubomoa na kuharibu kila kitu kilichokuwa juu ya makaburi ya mji wa Madina na nje ya mji huo. Miongoni mwa makaburi yaliyobomolewa na kuharibiwa vibaya ni makaburi manne ya maimamu na wajukuu wa Mtume (s.a.w), makaburi ya Abdullah na Amina, wazazi wa mtukufu Mtume (s.a.w), kaburi la Ibrahim mtoto wa kiume wa Mtume (s.a.w) na kaburi la Ummul Banin mke mwema wa Imam Ali bin Abi Twalib na makaburi ya masahaba wa Mtume (saw). Kaburi pekee lililobakishwa na Mawahabi hao wenye mioyo ya kikatili ni la Mtume Muhammad (s.a.w), kwani walijua kuwa kubomoa kaburi la mtukufu huyo kungezua hasira kali ya Waislamu duniani.

Makaburi ya maswahaba wa Mtume ya Baqii yalibomolewa na mawahabi wa Saudi Arabia

Siku kama ya leo miaka 113 iliyopita inayosadifiana na 3 Julai 1904, alifariki dunia Theodor Herzl, mwasisi wa harakati ya Kizayuni. Herzl alizaliwa mwaka 1860 mjini Bucharest mji mkuu wa Hungary na kisha kuelekea Austria. Mnamo mwaka 1897 aliasisi Taasisi ya Kimataifa ya Kizayuni kwenye kongamano lililofanyika nchini Uswisi. Herzl alibuni mikakati ya kuasisiwa utawala ghasibu na wa Kizayuni wa Israel kwenye ardhi za Palestina, utawala ambao hadi leo unaendelea kufanya jinai kubwa na kusababisha maafa yasiyo na kifani dhidi ya raia madhlumu wa Palestina.

Theodor Herzl

Na miaka 114 iliyopita katika siku kama ya leo ambayo ni sawa na tarehe 8 Shawwal mwaka 1324 Hijria toleo la kwanza la gazeti la 'Majlis' lichapishwa nchini Iran. Gazeti hilo lilianzishwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Mirza Sayyid Muhammad Sadiq Tabatabai. Mbali na gazeti hilo kuandika habari za ndani na nje ya nchi, liliakisi pia mazungumzo yote ya Majlisi ya Ushauri ya Iran yaani Bunge.

Gazeti la Majlis