Jan 07, 2019 13:23 UTC
  • Sayansi na Teknolojia Mpya (23)

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala hii ambayo huangazia mafanikio katika uga wa sayansi na teknolojia duniani na nchini Iran.

Kwa mujibu wa ripoti wa ripoti za hivi karibuni, kiwango cha ustawi wa kila mwaka wa makala za sekta za sayansi ya uhandisi duniani kiliongoezeka kwa asilimia 6 katika kipindi cha muongo moja uliopita. Lakini katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kiwango hicho kiliongezeka kwa asilimia 22 na hivyo kuifanya nchi hii kuwa iliyostawi zaidi katika uga huo wa kielimu duniani.

Baada ya Iran, nchi zilizofuata ni China na India ambazo ustawi wao katika uga huo ulikuwa ni wa asilimia 14 na kufuatia na nchi za Brazil, Korea Kusini, Australia, Uhispania, Italia, Russia na Canada kwa taratibu.

@@@

www.natureindex.com ni tovuti ambayo huchapisha na kusamabaza makala ya kiutafiti kutoka majrida yenye itibari zaidi duniani baada ya kufanya uchunguzi wa kina. Kila mwezi hufanyika mabadiliko katika tovuti hiyo ambapo makala za punde zaidi huwa zinawekwa kwa ajili ya kuwafikia wasomaji kote duniani. Kwa mujibu wa msimamizi wa tovuti hiyo yenye itibari, katika ulimwengu wa Kiislamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio nchi iliyowekeza kwa kina katika uga wa sayansi na teknolojia za kistratijia kama vile seli shina, nishati mpya, biotekonolojia, teknolojia ya mikroeletroniki, anga za mbali, teknolojia ya nano na tiba ya mimea. Aidha Iran imetajwa kuwa sasa miongoni mwa nchi zinazoongoza katika sayansi muhimu duniani.

Iran yashika nafasi ya kwanza ya sayansi na teknolojia


Utafiti mpya uliochapishwa mwezi Oktoba na muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa lililojikita na masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), umetathimini kwa kina mchango wa ICT katika uchumi wa mataifa mbalimbali.

Utafiti huo “Mchango wa kiuchumi wa kanuni za brodbandi, masuala ya kidijitali na ICT” unasema  ongezeko la matumizi ya brodbandi yanaleta  nuru katika ukuaji wa uchumi.

Ukigeukia mabadiliko ya kidijitali utafiti huo unaonyesha kwamba mchango wa kiuchumi wa kukumbatia mabadiliko hayo ni mkubwa, sawa na ule unaoletwa na matumizi ya brodband kupitia simu za rununu au simu za kiganjani.

Utafiti pia umebaini kwamba sera muafaka na zinazofanya kazi pamoja na mikakati bora vinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kupitia mfumo wa kidijitali. Na kwa mantiki hiyo Houlin Zhao katibu mkuu wa ITU amesema “kwa utafiti huu wa kihistoria sasa tunaweza kuthibitisha matokeo ya usambazaji wa broadband na mabadiliko ya kidijitali katika ukuaji wa uchumi, na kwamba uwekezaji katika miundombinu ya ICT ni kipaumbele cha kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za broadband, na pia kusaidia kuharakisha mafanikio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu au SDG’s."

Kwa mujibu wa ITU utafiti huo pia umesema kupitia mfumo ambayo ni mifano ya kuigwa, kanuni pamoja na mpango wa kuchunguza athari za kiuchumi za broadband na kuwezesha uchambuzi kamili wa takwimu za mabadiliko ya kidigital kutasaidia kutoa ushahidi kwa kuzingatia uundwaji wa sera a maendeleo yanayopatikana.

Teknolojia maalumu iliyobuniwa na watafiti wa Kiirani kuchoma vyobo vya plastiki

 

Wanafunzi Wairani mapema mwezi Novemba walishika nafasi ya kwanza katika Mashindano ya 12 ya Kimataifa ya Elimu ya Nujumu na Fizikia ya  Elimu ya Nujumu- IOAA- nchini China.

Kwa mujibu wa taarifa, wanafunzi Wairani walipata medali za dhahabu katika mashindano yaliyofanyija Beijing kuanzia Novemba 3 hadi 11.  Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kuwaleta pamoja wanafunzi bora zaidi katika taaluma ya nujumu duniani. Mashindano hayo yalianza nchini Thailand mwaka 2006 kwa ubunifu wa Poland, China, Iran, Indonesia na Thailan na hufanyika kwa lengo la  kuwatia motisha wanafunzi wa shule za upili wanaovutiwa na elimu ya nujumu. Aidha mashindano hayo hulenga kuimarisha urafiki na ushirkiano baina ya wanafunzi hao wa taalauma ya nujumu kwa ajili ya ustawi wa taaluma hiyo katika siku za usoni.

Spika wa Bunge la Iran, Ali Larijani aliwatumia wanafrunzi hao salamu za pongezi kufuatia ushindi huo. 

@@@

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshiriki katika Maonyesho ya 20 Teknolojia ya China maarufu kama China Hi-Tech Fair ambayo yalifanyika Novemba 19 hadi 21 katika mji wa Shenzen kusini mwa China.

Mashirika manne ya Iran ambayo msingi wake ni elimu na utafiti yaani knowledge-based yalishiriki katika maonyesho hayo ambapo yamewasilisha mafanikio yo katika uga wa Intaneti ya Vitu au IoT.  Hii ni intaneti ambayo huwa imeunganishwa na vitu ambavyo mwandamu hutumia kila siku ili kuviwezesha kutuma na kupokea data. Aidha  mashirika hayo ya Iranyalioneysha mafanikio yaliyopatika katika uga wa Artificial Intelligence yaani kompyuta kuwa na uwezo wa kufikiria kama mwanadamu.

Maonyesho hayo yalishirikisha mashirika 3,500 ya China pamoja na mashirika mengine kutoka nchi 30 ambayo yalionyesha mafanikio yao katika nyuga mbali mbali na ubinifu katika anga za mbali, roboti pamoja na ustawi wa miji na afya. Maonyesho ya Teknolojia ya China maarufu kama China Hi-Tech Fair ni maonyesho muhimu na bora zaidi ya teknolojia nchini China.

@@@

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi sasa imefanikiwa kuuza bidhaa zake za teknolojia ya nano katika nchi 50 duniani.

Hayo yamedokezwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Idara Maalumu ya  Iran ya Masoko ya Nano Teknolojia Reza Asadi-Far. Huku akiashiria mafanikio ya wanasayansi Wairani katika uga wa teknolojia ya nano, ameendelea kusema kuwa:  "Idadi ya bidhaa ambazo msingi wake ni teknolojia ya nano nchini Iran ziliongezeka kutoka 13 mwaka 2008 hadi 494 katika mwaka huu wa 2018."

Aidha ametabiri kuwa kutashuhudiwa ongezeko kubwa la bidhaa za teknolojia ya nano kutoka Iran ambazo zinaozuwa katika masoko ya kimataifa. Amezitaja baadhi ya nchi ambazo zinanunua bidhaa za teknolojia ya nano kutoka Iran kuwa ni pamoja na Iraq, Uturuki, Georgia, India, Afghanistan, Turkmenistan, Jamhuri ya Azerbaijan, Armenia na China

Watafiti wa Kichina watengeneza masikio ya watoto watano kwa mara ya kwanza

 

Na mwezi wa Novemba Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilizindua kwa mra ya kwanza nchini duka la dawa ambalo linatumia roboti kuwahudumia wateja katika mji wa Oroumiyeh kaskazini magharibi mwa Iran.

Hilo ndilo duka la kwanza kabisa la dawa lenye kutumia roboti nchini Iran na litatumika katika kituo cha afya.

Duka hilo la dawa liko katika Kiliniki Maalumu ya Tadbir na limejengwa katika eneo lenye ukubwa wa kilomita mraba 26,000.

Kwa mujibu wa taarifa duka hilo linaweza kuwahudumia wateja 12 katika kipindi cha dakika moja na kutoa madawa 8,000 katika kipindi cha dakika 60.

@@@@

Naama wapenzi wasikilizaji na kwa mafanikio hayo ya Iran kuzindia duka la dawa ambalo huduma zake zote zinatolewa na roboti ndio tunafika mwisho wa makala yetu ya sayansi an teknolojia leo. Ni Matumaini yetu kuwa umwezeka kunufaika. Hadi wakati mwinginen panapo majaliwa yake mola, Kwaherini.