Jul 15, 2020 02:52 UTC
  • Jumatano tarehe 15 Julai 2020

Leo ni Jumatano tarehe 23 Dhulqaada 1441 Hijria inayosadifiana na Julai 15 mwaka 2020.

Siku kama ya leo miaka 116 iliyopita, alifariki dunia Anton Chekhov, mwandishi mashuhuri wa visa wa karne ya 19 wa Urusi akiwa na umri wa miaka 64. Chekhov alikuwa tabibu na katika kujitolea alijenga kituo cha tiba ambacho alikitumia katika shughuli hiyo. Baada ya hapo alijiunga na taaluma ya uandishi ambapo alianza kujishughulisha na kazi za uandishi katika magazeti na kuandika makala tofauti wakati huo. Alikuwa mahiri katika tenzi fupifupi na akatokea kuwa mashuhuri katika uga huo. Miongoni mwa athari za mwandishi huyo ni pamoja na kitabu cha "Jogoo wa Bahari".

Anton Chekhov

Siku kama ya leo miaka 100 iliyopita, mfalme wa Syria aliyewekwa katika nafasi hiyo na Uingereza alifanikiwa kuwa mfalme wa Iraq baada ya kukimbia kutoka Damascus. Julai 15 mwaka 1920, baada ya vikosi vya Ufaransa kukaribia mji wa Damascus, Amir Feisal aliyekuwa ametawalishwa na Uingereza huko nchini Syria aliukimbia mji huo. Syria na Lebanon ni miongoni mwa ardhi zilizokuwa chini ya mamlaka ya utawala wa Othmania ambazo mwishoni mwa Vita vya Kwanza vya Dunia ziliwekwa chini ya udhibiti wa Ufaransa. Tarehe 18 Julai mwaka huo huo, mji wa Damascus ulitekwa na kukaliwa kwa mabavu na vikosi vya Ufaransa. Amir Feisal ambaye aliongoza Syria kwa miezi mitatu tu akiwa Mfalme, baadaye akatawalishwa na Uingereza kuwa Mfalme wa Iraq.

Amir Feisal

Siku kama ya leo miaka 76 iliyopita inayosadifiana na tarehe 15 Julai mwaka 1944, jeshi la Marekani lilianza kuishambulia Japan kwa maelfu ya mabomu yaliyodondoshwa na kurushwa na ndege kubwa aina ya B-29 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Mashambulio hayo ya mabomu ya Marekani yaliendelea hadi Japan iliposalimu amri mbele ya majeshi ya Marekani. Tukio hilo chungu licha ya kusababisha makumi ya maelfu ya wananchi wasio na hatia wa Japan kuuawa kwa halaiki, lilipelekea pia zaidi ya viwanda elfu tatu vikubwa na vidogo kuharibiwa kabisa nchini humo.

Vita vya Pili vya Dunia

Siku kama ya leo miaka 62 iliyopita, Nuri Said Pasha Waziri Mkuu wa zamani wa Iraq aliuawa baada ya kujiri mapinduzi ya umwagaji damu. AlijIunga na jeshi la utawala wa Othmania akiwa na umri wa miaka 21 na kushiriki katika vita vya utawala wa Othmania na Bulgaria vilivyojiri mwaka 1912. Nuri Said Pasha sambamba na kuwa mwanajeshi, alianzisha harakati za kisiasa na alizingatiwa na Uingereza wakati wa malalamiko ya kisiasa dhidi ya utawala wa Othmania. Hatimaye mwaka 1930 akipata himaya ya Uingereza alichaguliwa kuwa waziri Mkuu wa Iraq.

Nuri Said Pasha

 

Tags