Jul 13, 2022 06:23 UTC
  • Jumatano tarehe 13 Julai 2022

Leo ni tarehe 13 Dhulhija 1443 Hijria sawa na tarehe 13 Julai 2022.

Siku kama ya leo miaka 1958 iliyopita, moto mkubwa ulitokea huko Roma mji mkuu wa utawala wa kifalme wa Roma. Sehemu kubwa ya mji wa kihistoria na mkongwe wa Roma iliungua na wakazi wengi wa mji huo walipoteza maisha yao kutokana na moto huo. Moto huo ulikuwa kisingizio tosha kwa Nuren mtawala mmwagadamu wa Kirumi ambaye aliwauwa kwa umati watu zaidi ya laki moja na baadaye kuwatuhumu Wakristo kuwa ndio walioanzisha moto huo.

Miaka 622 iliyopita katika siku kama ya leo, liliundwa jeshi la kale zaidi duniani nchini Uswisi. Jeshi hilo la kale zaidi duniani hadi hii leo limebakia kama lilivyokuwa na hata mavazi ya wanajeshi wake hayajabadilika. Idadi ya wanajeshi wa jeshi hilo dogo lakini lenye nidhamu kubwa ni watu 83. Jeshi hilo ambalo wanachama wake daima huwa raia wa Uswisi, liliundwa kwa ajili ya kulinda viongozi wa Kikatoliki wa wakati huo na hii leo baada ya kupita zaidi ya miaka zaidi ya 600 tangu liundwe, jeshi hilo lina jukumu la kumlinda Papa wa Kanisa Katoliki huko Vatican.

Bendera ya Uswisi

Katika siku kama ya leo miaka 251 iliyopita, baharia na nahodha mashuhuri wa Kiingereza aliyejulikana kwa jina la James Cook alikamilisha safari yake ya kitafiti na kielimu ya kuelekea The Great Southern Continent. Safari hiyo ilikuwa imeanza tarehe 26 Julai mwaka 1768. Safari hiyo ndefu iliishirikisha pia timu ya watalaamu wa elimu ya Sayansi Asilia au Natural Science kwa kimombo. Wataalamu hao walikuwa na nia ya kufanya utafiti wa kielimu kuhusiana na mimea pamoja na viumbe wanaopatikana katika maeneo hayo.

James Cook

Katika siku kama ya leo tarehe 13 Dhulhija miaka 54 iliyopita, alifariki dunia mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu Allamah Agha Bozorge Tehrani. Alipata elimu ya msingi mjini Tehran na baadaye alielekea Najaf, Iraq kwa ajili ya elimu ya juu. Allamah Agha Bozorge Tehrani alikwea kwa kasi daraja za elimu na kuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa kidini. Allamah Tehrani alisafiri na kufanya uchunguzi katika maktaba nyingi za maeneo mengi kama Iran, Misri, Syria, Iraq, Hijaz, Palestina na kadhalika kwa ajili ya kutayarisha ensaiklopedia ya vitabu vya Kiislamu. Alifanikiwa kuandika tabu hilo kubwa lenye juzuu 26 ambalo alilipa jina la "Al Dhari'a ila Tasaanifish Shia". Kitabu kingine muhimu cha Allamah Agha Bozorge Tehrani ni "Tabaqatu A'lami al Shia" chenye juzuu 8. Msomi huyo mkubwa wa Kiislamu alifariki dunia katika mji mtakatifu wa Najaf na kuzikwa katika maktaba yake kama alivyokuwa ameusia. 

Allamah Agha Bozorge Tehrani (katikati)

Miaka 31 iliyopita katika siku kama ya leo ya tarehe 22 Tir 1370, Hijria Shamsia aliaga dunia, Allamah Sayyid Tahir Sayyidzadeh Hashemi, mmoja wa wanafikra wa Kiirani. Aliaga dunia katika viunga vya mjii wa Kerman ulioko magharibi mwa Iran. Katika kipindi chote cha maisha yake, Sayyyidzadeh Hashemi alijishughulisha na uenezaji na usambazaji wa maarifa ya Kiislamu kupitia kufundisha na kulea wanafunzi wa masomo ya dini, kutoa mawaidha na kuandika vita.  Kwa hakika alimu huyu ametoa huduma kubwa katika uwanja huu. Allamah Sayyidzadeh Hashemi alikuwa ametabahari pia katika fani ya hati. Alimu huyo alikuwa akizifahamu vizuri na kikamilifu lugha za Kiarabu, Kifarsi na Kikurdi na alikuwa mahiri pia katika utunzi wa mashairi na ameacha athari nyingi katika uwanja huo kwa lugha hizo tatu.

Allamah Sayyid Tahir Sayyidzadeh Hashemi

Na tarehe 13 Julai inayosadifiana na Jumamosi ya leo ni siku ya kumbukumbu ya  Romania kujipatia uhuru kutoka kwa Utawala wa Othmania. Kijiografia Romania ipo kusini mashariki mwa Ulaya na magharibi mwa Bahari Nyeusi. Romania ina zaidi ya wakazi milioni 22 na dini rasmi ya nchi hiyo ni Ukristo na madhehebu ya Othodox ndiyo yenye wafuasi wengi. Nchi hiyyo ilikuwa chini ya utawala wa Othmania kuanzia karne yay 15. Hata hivyo mwaka 1877 Romania ikaungana na Russia katika vita dhidi ya utawala wa Othmania. Hatimaye katika siku kama ya leo Romalia ikajipatia uhuru na miaka mitatu baadaye ikawa imepata uhuru kamili.

Bendera ya Romania

 

Tags