Mar 27, 2023 02:10 UTC
  • Jumatatu, tarehe 27 Machi, 2020

Leo ni Jumatatu tarehe 5 Ramadhani 1444 Hijria sawa na Machi 27 mwaka 2023.

Siku kama ya leo miaka 526 iliyopita, alizaliwa Hans Holbein the Younger, mchoraji wa Ujerumani katika familia ya kisanii. Younger alijifundisha sanaa ya uchoraji kutoka kwa baba yake aliyekuwa mashuhuri katika uwanja huo. Baada ya hapo alielekea nchini Uswisi na kuvisaidia vyombo vya usalama katika shughuli ya kuonyesha taswira za watu hususan wahalifu. Baada ya muda, alielekea Uingereza na kuendelea na kazi yake hiyo na kupata umaarufu mkubwa. Hans Holbein the Younger alifariki dunia mwaka 1543.

Hans Holbein the Younger

Siku kama ya leo miaka 178 iliyopita alizaliwa Wilhelm Conrad Rontgen, mwanafizikia na mwanasayansi maarufu wa Ujerumani. Mwaka 1845 aligundua miale ya X na mwaka 1901 alitunukiwa tuzo ya Nobel kwa kufanikiwa kugundua miale hiyo. Kwa kuwa hakutambua miale aliyoigundua, Rontgen aliamua kuipa jina la X. Miale hiyo hupenya kwa urahisi katika mwili wa mwanadamu na kwa sababu hiyo ni njia nzuri zaidi ya kuchukua taswira ya viungo au picha ya X-ray inayotumiwa kujua sehemu za ndani ya mwili zilizodhurika au kuvunjika.

Wilhelm Conrad Rontgen

Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita inayosadifiana na 27 Machi 1948, serikali ya Ufaransa iliasisi jumuiya iliyozishirikisha Ufaransa na nchi waitifaki, pamoja na nchi ambazo zilikuwa makoloni ya nchi hiyo kwa kuzikutanisha pamoja nchi hizo. Muungano wa nchi hizo unafanana na ule wa Jumuiya ya Madola, ambao unazijumuisha nchi zilizowahi kutawaliwa na Uingereza. Kuundwa kwa muungano huo ulikuwa mwanzo wa kuandaliwa mazingira ya kuundwa Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa 'Francophonie' ambayo iliasisiwa mwaka 1970. Wanachama wengi wa jumuiya hiyo wanatoka barani Afrika.

Miaka 55 iliyopita katika siku kama hii ya leo alifariki dunia mwanaanga wa kwanza duniani Yuri Gagarin. Baada ya kuhitimu masomo na kuchaguliwa katika klabu ya masuala ya anga ya Urusi ya zamani, Gagarin alijiunga na programu ya masuala ya anga ya Urusi ya zamani na kuteuliwa kati ya watu 20 waliotakiwa kufanya mazoezi ya kutumwa angani. Tarehe 12 Aprili 1961 Yuri Gagarin alipanda kwenye roketi la Vostok 1 na kuwa mwanadamu wa kwanza kutumwa katika anga za mbali. Siku hiyo Gagarin aliyekuwa na umri wa miaka 27 aliizunguka dunia kwa dakika 89. Gagarin alifariki dunia akiwa pamoja na mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa sekta ya masuala ya anga wa Urusi ya zamani katika ajali ya ndege hapo mwaka 1968.

Yuri Gagarin

Siku kama hii ya leo miaka 35 iliyopita Katibu Mkuu wa wakati huo wa Umoja wa Mataifa alitoa taarifa akilaani kitendo cha utawala wa Iraq cha kutumia silaha za kemikali katika vita vyake dhidi ya Iran. Baada ya kupita muda serikali ya Iraq ikitumia silaha za kemikali na kutochukuliwa hatua ya maana katika Baraza la Usalama ya kukabiliana na suala hilo, Katibu mkuu wa wakati huo wa Umoja wa Mataifa, Javier Pérez de Cuéllar alichukua hatua ya kutoa taarifa yake mwenyewe akiilaani Iraq kwa kutumia silaha za kemikali licha ya kimya cha Baraza la Usalama. Javier Pérez de Cuéllar alisema katika taarifa yake iliyotolewa tarehe 28 Machi 1988 kwamba: "Kuna ushahidi mwingi unaothibitisha kwamba jeshi la Iraq linatumia silaha za kemikali ambazo zimesababisha madhara makubwa kwa raia wa Iran na Iraq." Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa alisema: utumiaji wa silaha za kemikali umapaswa kulaani. 

Javier Pérez de Cuéllar

 

Tags