Watumiaji wa X: Hamas inawakilisha watu wa Palestina
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wameitaja harakati ya muqawama wa Palestina "Hamas" mwakilishi wa watu wa Palestina wanaotetea taifa lao.
Siku ya Jumanne, Septemba 9, ndege za kivita za Israel zilikiuka anga ya Qatar na kushambulia maeneo yaliyolengwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Doha. Mahali palipotokea mlipuko huo ndipo palipokuwa mkutano wa ujumbe wa ngazi za juu wa Hamas uliokuwa ukiongozwa na Khalil al-Hayyah katika eneo la Electra.
Kuhusiana na hilo, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X nao waliunga mkono harakati hiyo baada ya utawala wa Israel kuishambulia Qatar kwa lengo la kuiangamiza Hamas.
"Fatma" kutoka mtandao wa kijamii wa X aliandika: "Hamas inatetea nchi yake, Palestina, na inawakilisha watu wa nchi hii. Lakini utawala ulioikalia kwa mabavu ardhi ya Palestina na kuwauwa shahidi zaidi ya watu 64,000 ni gaidi."
"Ali Mardani," mtumiaji mwingine wa X, aliwahutubu Wazayuni: "Mnapoikalia ardhi kwa takriban miaka 80, mkifanya mauaji ya halaiki na uhalifu, mnatarajia Hamas, ambayo inawaungwa mkono na inatokana na watu wa Gaza, iwape shada la maua?!"
! Udanganyifu wa uwongo! Haya ni majibu tupu. Hakuna mtu atakayedanganywa nawe tena!”
"Mukarama" pia amesema kwamba hata kukaliwa kabisa kwa Gaza sio hakikisho la kushindwa kwa Hamas na kwamba harakati hii bado inafanya kazi zaidi ya mahesabu ya kijeshi.
"Atiyeh Bakhtiari" pia alisema, alipoulizwa ni kwa nini Hamas haitajisalimisha kwa Israel: "Kwa sababu suala hilo si kundi moja. Suala ni ukaliaji na ukandamizaji wa taifa. Hamas haitajisalimisha kwa sababu haitaruhusu taifa la Palestina kuangamizwa."
Mtumiaji mmoja aitwaye "Majid" aliandika, akizungumzia kushindwa kwa utawala wa Kizayuni kufikia malengo yake, ikiwa ni pamoja na kuangamizwa Hamas huko Gaza: "Utawala huo hauwezi kuikalia Gaza wala kuiangamiza Hamas. Utawala huu umezama katika kinamasi kiasi kwamba hauwezi hata kuwakomboa mateka wake."
"Seyed Ali Akbar Razavian" anaichukulia Hamas kuwa ndiyo inayofichua maovu na jinai za Israel na mshirika wake Marekani, na amesema: "Kilichofungua macho ya walimwengu kuona jinai za Tel Aviv na Washington huko Gaza na kuwafichua washirika hao wawili kwa walimwengu ni muqawama wa Hamas pamoja na watu wa Gaza."