Jan 09, 2023 10:02 UTC
  • Sifa za kipekee za Kamanda Qassem Soleimani

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kuwa nami katika sehemu nyingine ya vipindi maalumu vinavyokuijieni kwa mnasaba wa kukumbuka tukio la kuuliwa kigaidi aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Meja Jenerali Qasem Soleimani. Leo tunazungumzia sifa za kipekee za kamanda huyo aliyeuwa katika hujuma ya kigaidi ya jeshi la Marekani akiwa safarini nchini Iraq.

Miaka 3 imepita tangu kuuawa shahidi kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Shahidi Meja Jenerali Haj Qassem Soleimani. Haj Soleimani alikuwa mtu mkubwa ambaye hakujali chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika kutekeleza wajibu wake. Watu wengi wa eneo la Asia Magharibi na ulimwengu kwa ujumla wanamtambua Shahidi Qassem Soleimani kama shujaa aliyekuwa na mchango adhimu katika vita dhidi ya makundi na kitakfiri n kigaidi kama Daesh (ISIS). Ushujaa wa Haj Qasim ni mojawapo ya vipengele vya sifa zake makhsusi ambazo, pamoja na sifa nyinginezo za kibinafsi, alikuwa mtu anayempenda sana na kumuashiki Mwenyezi Mungu SW. 

Luteni Jenerali, Shahidi Haj Qassem Soleimani 

Haj Qassim alikulia katika shule ya Uislamu. Shule hiyo ya Uislamu humuona mtu kamili kuwa ni yule aliyekamilika katika pande zote na si katika upande mmoja tu. Kwa mtazamo wa Uislamu, mtu hawi mkamilifu kwa kujifunza sayansi tu, au kwa kuvaa vazi la kujinyima raha na uchamungu pekee, au anayejikita katika fani ya siasa na kukanyaga haki na uadilifu kwa jina la kutetea maslahi ya taifa. Watu walioelimika na kukulia katika shule ya Uislamu ni watu wenye shakshia nyingi, kama alivyokuwa Haj Qasim Soleimani. Meja Jenerali Soleimani alilelewa katika shule ambayo ndani yake masuala ya kiroho hayamzuii kuwa mwanasiasa mwadilifu, wala siasa haimuondoi katika njia ya maadili mema na uchamungu. Alikuwa akisema: Nina huzuni kwamba kwa nini tunaachana na kusahau maadili katika siasa. Kwani uchamungu na maadili unapaswa kuonekana wapi? Kwa nini tunasahau kuwa wachamungu tunapoingia kwenye siasa? Na kwa nini tunasahau siasa tunapoingia kwenye uchamungu?

Shahid Qassem Soleimani hakuwa mwanajeshi na mtu wa masuala ya usalama tu. Sifa ya kwanza muhimu sana na kubwa ya maisha ya Haj Qasim ilikuwa ikhlasi yake. Anasema katika barua aliyomwandikia mmoja wa makamanda wa kikosi cha Tharullah kwamba: “Ali, usisahau mambo manne: Muhimu zaidi, ni ikhlasi, ikhlasi, ikhlasi, kwa maana ya kusema, kutenda au kutotenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Ondoa kila kitu moyoni mwako isipokuwa Yeye SW na uujaze upendo Wake Allah na Ahlul-Bait wa Mtume Muhammad (saw).

Jenerali Qassem Soleimani, kama walivyokuwa mashahidi wenzake wengi, alikuwa na hakika kwamba nguvu zao haziko katika wingi wa vifaa na zana zao za kijeshi, bali katika kiasi na kadiri ya uhusiano wao na Mwenyezi Mungu SW. Mola Mlezi alikuwa kitovu na msingi wa kazi zote za Haj Qasim.

Alipenda sana kufanya ibada nyakati za usiku na daima alikuwa akiswali, kumuomba na kumhimidi Allah Jalla Jalaaluh katika nyakati hizo. Aliamini kwamba watu wote ambao wamefika kwenye daraja za juu za ukamilifu, hasa wa kiroho na hata wa kidunia, chanzo chake ni kukesha usiku kwa ajili ya ibada. Alikuwa akisoma sana Qur'ani tukufu na kuzingatia Aya zake. Alikuwa na Qur'ani ndogo mfukoni mwake na alitumia wakati kadiri ilivyowezekana kuisoma, hata alipokuwa ndani ya teksi. Usishangae kusikia kwamba Shahidi Qassem Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds, alikuwa akitumia teksi mara nyingi kwenda sehemu tofauti bila mlinzi. Chanzo na msingi wa utulivu wake wa kiroho na ushujaa wake mkubwa ulikuwa katika imani yake kubwa kwa Allah SW, kutawakkal na kumtegemea Yeye pekee na katika kuwa na yakini kwamba hakuna chochote kinachoweza kutukia isipokuwa kwa matakwa Yake. Kamanda Soleimani alimpenda sana Mtume Muhammad (saw) na Ahlubaiti wake, hususan binti yake kipenzi, Fatima Zahra (sa). 

Haj Qasim aliutambua ulimwengu kuwa ni hadhara ya Mwenyezi Mungu SW. Kwa sababu hiyo, aliona kuwa ni wajibu kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu hata katika medani za vita. Kwa mfano tu, wakati mji wa Al-Bukamal huko Syria ulipokombolewa na wakahitaji kutumia nyumba moja ya eneo hilo kwa ajili ya makao makuu ya jeshi, Haj Qasim aliamuru vyombo vyote vilivyokuwemo viwekwe na kufungiwa katika chumba kimoja ili mali ya mwenye nyumba isipatwe na madhara.

Mfano mwingine ni pale alipomwandikia barua mwenye nyumba aliyekuwa amekimbia makazi yake kutokana na vita huko Syria na kuiacha kwenye nyumba hiyo. Alisema katika barua hiyo kwamba: "Mimi ni ndugu yao mdogo, Qassem Soleimani. Bilas haka unanijua. Tumetoa huduma nyingi kwa Ahlusunna. Mimi ni Muislamu wa madhehebu ya Shia na nyingi ni Waislamu wa madhehebu ya Suni… Nimeelewa kutokana na nakala ya Qur'ani tukufu, kitabu cha Sahihi Bukhari na vitabu vingine vilivyomo hapa nyumbani kwako kwamba nyinyi ni watu wenye imani. Awali ya yote, nakuomba radhi na natumai utanisamehe kwa kutumia nyumba yako bila ruhusa. Pili, tuko tayari kulipa uharibifu wowote uliotokea kwenye nyumba yako. Tunafikiri tuna deni kwako kwa sababu tumekaa katika nyumba hii bila idhini yako. Hii hapa nambari yangu ya simu nchini Iran, natumai utapiga simu, niko tayari kufanya chochote unachotaka."

Kamanda Soleimani aliandika nambari yake ya simu ndani ya barua hiyo.

Haj Qasim aliamini kwamba, ibada muhimu zaidi inayomkurubisha mja kwa Mwenyezi Mungu ni kuwatumikia wanaadamu. Dukuduku lake kubwa lilikuwa wananchi na hali zao. Aliwapenda sana wananchi na watu wa kawaida. Alifuata sura na sira ya Amirul Muuminin Ali bin Abi Twalib (as) katika kusuhubiana na watu. Alifuata maagizo ya Amirul Muumin (as) ambaye alimwandikia barua gavana wake nchini Misri, Malik al Ashtar akisema:

فاخفض لهم جناحک و الن لهم جانبک و ابسط لهم وجهک و آیس بینهم فى اللحظه والنظره حتى لایطمع العظمإ فى حیفک لهم و لاییإس الضعفإ من عدلک بهم, فان الله تعالى یسإلکم معشر عباده عن الصغیره من اعمالکم و الکبیره والظاهره والمستوره فان یعذب فإنتم اظلم و ان یعف فهو اکرم

Kuwa mnyenyekevu, mpole na mkarimu, na mwenye tabasamu kwa watu wote. Watazame watu wote kwa jicho sawa ili wakuu katika jamii wasiwe na tamaa ya kuwadhulumu watu dhaifu, na watu dhaifu wasikate tamaa na uadilifu wako; kwa sababu Mwenyezi Mungu atakuulizeni nyinyi waja wake kuhusu amali zenu kubwa na ndogo, za dhahiri na zisizo dhahiri…   

Shahidi Qassem Soleimani alikutambua kuwatumikia waja wa Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo njia yenye nguvu zaidi ya kumkaribia Mola Muumba na alitumia sehemu kubwa ya maisha yake katika njia hiyo. Tabia na mwenendo wa Haj Qasim kwa watu haikubadilika tangu alipokuwa mpiganaji wa kawaida hadi alipokuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC. Hadi anauawa shahidi, mienendo yake na watu wa ilionekana kama ya mwanakijiji aliyeingia jeshini mwaka 1980 ili kulinda thamani na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu. Jenerani aliendelea kuwa mpiganaji anayeshika bunduki na kupambana na adui katika mstari wa mbele wa medani za vita akiwa pamoja na wanamgambo na wapiganaji wa kawaida. 

Luteni Jenerali Shahidi Haj Qassem Soleimani 

Haj Qassem alikuwa mpole na mtulivu na hakukubali kutengewa sehemu na nafasi maalumu katika maeneo aliyokwenda. Alikuwa akiketi chini kwenye ardhi pamoja na askari na wapiganaji wengine na akila chakula pamoja nao. Alipumzika sehemu na maeneo yale yale ya wapiganaji wa kawaida. Hata kwenye mstari wa mbele vita, wakati mwingine alilala chini nyuma ya jiwe na kupumzika. Alikuwa mtu mwenye bidii na mwenye kujituma sana. katika operesheni za vita, wakati mwingine alikuwa akifanya mikutano ya kikazi kwa saa 19 kati ya saa 24 kwa siku. Wakati fulani alikuwa na mikutano mingi hata makamanda wenzake wa jeshi wakahoji, kamanda atalala lini? Katika siku za mwishoni mwa maisha yake, masahabu zake walisema kwamba Haj Qasim alikuwa akilala masaa mawili hadi matatu tu usiku katika vita vya kupambana na Daesh nchini Iraq.

Jenerali Qassem Soleimani alipenda sana kusoma vitabu. Alisoma vitabu vyenye maudhui mbalimbali na daima alikuwa akiwaasa wenzake kusoma na kutalii vitabu. Vilevile alitumia baadhi ya wakati kuandika.  

Licha ya kazi zake nyingi lakini Kamanda Soleimani kamwe hakuwasahau watu aliokuwa nao katika medani za vita vya miaka nane ya kujitetea kutakatifu. Naser Tobeiha alikuwa mmoja wa makamanda wa Kikosi cha 41 cha Tharullah. Alijeruhiwa kwa kipande cha kombora katika operesheni ya Walfajr 4, na kuvunjika uti wa mgongo.

Siku moja, Kamanda Qassem Soleimani alikwenda kumtembelea. Alikaa naye kwa masaa kadhaa. Wakati anaondoka, alimwambia mke wa swahiba wake kwamba: Nimeamua kuja kumhudumia Nasser kila mwanzoni mwa mwaka. Tangu wakati huo hadi wakati wa kifo cha veterani na majeruhi huyo wa vita, Jenerali Soleimani alikuwa akienda Kerman kila mwaka kumhudumia kwa kipindi cha miaka 25. Kila mara alipokuwa akienda kuwawaona wazazi wake, Kamanda Soleimani alikuwa pia akienda nyumbani kwa Tobeyha, kumpikia, kumuogesha na kumtunza.

Shahidi Soleimani na Shahidi Tobeyha 

Meja Jenerali Qassem Soleimani aliishi maisha ya zuhudi na kuipa mgongo dunia. Ofisi yake haikuwa na tofauti na ofisi za wafanyakazi wa chini kabisa wa vikosi vya jeshi, bali ilikuwa duni na hakiri zaidi. Aliishi katika nyumba moja ndogo mjini Tehran katika kipindi cha miaka 21. Kamera zilizoruhusiwa kuingia nyumbani kwake baada ya kuuawa shahidi zilionyesha picha ambazo baadhi ya watu waliuliza kwa mshangao iwapo nyumba hiyo na vyombo vilivyokuwemo vilikuwa vya Kamanda Soleimani au la?!!.