Pars Today
Leo ni Jumanne tarehe 25 Rabiuthani 1438 Hijria sawa na Januari 24, 2017.
Leo ni Ijumaa tarehe 21 Mfunguo Saba Rabiuthani 1438 Hijria sawa na Januari 20, 2017 Milaadia
Assalamu Alaykum Wapenzi wasikilizaji na karibuni kuwa nami tena katika sehemu nyingine ya makala hizo zinazokujieni kwa mnasaba wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja na Maulidi ya Mtume Muhammad (saw). Kipindi chetu leo kitazungumzia Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na fikra ya umoja baina ya Waislamu.
Tarehe 13 mwezi Aaban mwaka wa Hijria Shamsia ambayo mwaka huu inasadifiana na tarehe 3 Novemba, inatambuliwa hapa nchini Iran kama Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Ubeberu wa Kimataifa.
Waziri wa Ulinzi Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amesema taifa la Iran lingali limesimama imara katika misimamo yake ya kulinda thamani na malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, uchumi wa kimuqawama, utamaduni na kufuatilia siasa za ndani ya nchi, za kieneo na za kimataifa ndivyo vipaumbele vikuu vya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran).
Profesa Richard Falk, mhadhiri wa Sheria za Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Princeton na ripota maalumu wa zamani wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya haki za binadamu Palestina amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni tukio kubwa na la kipekee katika karne ya 20.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: "Chuo cha kidini (Hawza) mjini Qum kinapaswa kubakia "Chuo cha Kimapinduzi na Chimbuko la Mapinduzi" na ili kufikia lengo hilo kuna haja ya kuwepo fikra, tadbiri na mpango wa kina."
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kujitokeza kwa wingi na kwa mwamko wananchi wa Iran katika chaguzi mbili zijazo za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na ule wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu la kumchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu kutabatilisha njama za maadui.