Dehqan: Taifa la Iran litaendelea kulinda malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu
(last modified Tue, 16 Aug 2016 15:34:58 GMT )
Aug 16, 2016 15:34 UTC
  • Dehqan: Taifa la Iran litaendelea kulinda malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu

Waziri wa Ulinzi Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amesema taifa la Iran lingali limesimama imara katika misimamo yake ya kulinda thamani na malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya nne ya Sherehe za Kujitolea Mhanga zinazofanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kurejea nyumbani katika ardhi ya Kiislamu mateka waliokomboka wa vita vya miaka minane vilivyoanzishwa na utawala wa Ba'ath wa Iraq dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Hussein Dehqan

Brigedia Jenerali Dehqan amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yametoa somo la kihistoria kwa mataifa na kutekeleza harakati kubwa katika kalibu ya kutetea uhuru na kujitawala kwa mataifa.

Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza juu ya kulindwa thamani za Mapinduzi ya Kiislamu na kueleza kwamba katika miaka iliyopita wananchi wa Iran wameweza kuulinda Uislamu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuweza kuwadhihirishia walimwengu nguvu za Uislamu.

Baadhi ya mateka waliokomboka wa vita waliohudhuria sherehe hizo

Brigedia Jenerali Dehqan ameashiria uafriti na vizuizi vinavyowekwa na Marekani katika utekeelzaji wa makubaliano ya nyukia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kubainisha kuwa: JCPOA umevunja mpango wa maadui wa kuendeleza sera za kueneza hofu juu ya Iran; na leo hii hakuna nchi yoyote inayoiangalia Iran kama kitu hatari duniani.

Sambamba na kubainisha kuwa ngome za muqawama ambazo zimejitokeza leo katika nchi za Yemen, Syria, Iraq na sehemu nyengine duniani kukabiliana na mfumo wa Ubeberu zimepata ilhamu kwa Mapinduzi ya Kiislamu, Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema ikiwa mataifa yatakuwa na imani na malengo yao matukufu yatapata ushindi tu.../

 

Tags