Jan 17, 2021 07:52 UTC
  • Trump ampa Mfalme wa Morocco tuzo kwa kuanzisha uhusiano na Israel

Rais Donald Trump wa Marekani amemtunuku tuzo ya kifahari Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco, kutokana na hatua yake ya kukubali kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Y Net News, Trump amempa mtawala huyo wa Morocco tuzo inayofahamika kama 'Legion of Merit' ambayo hutolewa kwa nadra sana na rais wa Marekani na kuwapa marais au viongozi wa serikali wa nchi nyingine.

Hivi karibuni pia, Trump alipewa tuzo ya juu kabisa ya utawala wa Morocco, eti kutokana na jitihada zake za kufanikisha mpango wa kuanzisha uhusiano baina ya Morocco na utawala haramu wa Israel.

Trump alikabidhiwa tuzo hiyo ya 'Order of Muhammad' na Bintimfalme Lalla Joumala Alaoui katika sherehe ya faragha iliyofanyika katika Ikulu ya White House.

Trump (katikati), Mfalme wa Morocco kushoto na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Issrael

Aidha mkwe wa Trump ambaye pia ni mshauri mkuu wa rais huyo anayeondoka wa Marekani, Jared Kushner alipewa tuzo na Bintimfalme huyo kutoka kwa Mfalme wa Morocco, kutokana na mchango wake wa kufanikisha makubaliano ya kuanzisha uhusiano baina ya Morocco na Israel.

Mwezi uliopita wa Disemba, Trump alituma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter na kueleza kuwa Morocco na utawala wa Kizayuni wa Israel zimefikia mapatano ya kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia.

Kitendo hicho cha Morocco cha kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ambacho ni sawa na kusaliti malengo ya Palestina kimekabiliwa na radiamali hasi katika Ulimwengu wa Kiislamu na hata ndani ya Morocco kwenyewe. 

Tags