Jun 30, 2016 08:16 UTC
  • 18 waua katika shambulizi la bomu nchini Somalia

Kwa akali watu 18 wameripotiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu mapema leo katika mji wa Lafole, kusini magharibi mwa Somalia.

Abidkadir Mohamed, afisa mwandamizi wa polisi katika mji huo amethibitisha kutokea shambulizi hilo na kusema kuwa, basi dogo la abiria lilikanyaga bomo la kutegwa ardhini katika mji huo na kusababisha maafa hayo. Habari zaidi zinasema kuwa, gari moja lililokuwa na wafanyakazi wa serikali nyuma ya basi hilo ndilo lililolengwa kwenye hujuma hiyo ya kigaidi. Hadi tunaenda mitamboni, hakuna kundi lolote lililokuwa limekiri kuhusika na shambulizi hilo ingawa kundi la kigaidi la al-Shabaa limekuwa likitekeleza mashambulizi ya aina hii katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Watu zaidi ya 15 waliuawa Jumamosi iliyopita, katika shambulizi la kigaidi la wanamgambo wa al-Shabaab dhidi ya hoteli ya Nasa Hablod iliyoko katika mji mkuu Mogadishu, ambapo baada ya mripuko wa bomu wanamgambo hao waliingia eneo la tukio na kuanza kuwamiminia risasi watu waliokuwepo hotelini na kuwateka nyara wengine. Kwa mujibu wa polisi ya nchi hiyo, Buri Muhammad Hamza, Waziri wa Mazingira wa Somalia aliuawa katika shambulio hilo la mjini Mogadishu.

Tags