Nov 21, 2023 12:52 UTC
  • Maonyesho ya picha yafanyika Nairobi, Kenya kwa lengo la kuwaunga mkono watu wa Gaza

Waislamu na watetezi wa Palestina nchini Kenya wamefanya maonyesho ya picha na michoro inayoakisi matukio ya vita vya Gaza ili kuonyesha mshikamano na namna wanavyoumizwa na hali ya wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press, maonyesho ya picha na michoro yamefanyika katika ukumbi wa maigizo ya taifa wa Kenya mjini Nairobi, yakiakisi ukatili na unyama wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
 
Tukio hilo la kiutamaduni na sanaa limeandaliwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kenya na NGOs kwa lengo la kuwaunga mkono watu wa Ukanda wa Gaza likiwa ni kielelezo pia cha kusimama imara dhidi ya dhulma na udhalimu.

Watembeleaji wa maonyesho hayo ya Nairobi ya picha na michoro ya vita vya Gaza wameweza kufahamu dhulma na jinai za kinyama ambazo utawala ghasibu wa Kizayuni unawafanyia wananchi madhulumu wa Palestina na kuelewa pia ukweli ulivyo hivi sasa kuhusu vita vya Gaza.

Baada ya watetezi wa Palestina na Waislamu wa Kenya kubaini ukubwa wa jinai za kutisha zinazofanywa na Wazayuni huko Gaza kupitia athari za picha na michoro ya maonyesho ya Nairobi, walipatwa na mshtuko na kulaani mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayoendelea kufanywa na jeshi la Kizayuni.

Maonyesho ya Nairobi

Serikali ya Kenya inapinga kufanyika mikusanyiko na maandamano ya kulaani jinai za Wazayuni, lakini Waislamu na waungaji mkono wa Palestina nchini humo wamekuwa wakijitolea kuandaa matukio ya kiutamaduni na sanaa na kufanya vikao na mikutano mbalimbali kwa ajili ya kuwaunga mkono watu wanaodhulumiwa katika Ukanda wa Gaza.../

Tags