Jan 05, 2024 11:55 UTC
  • Rwanda yasitisha matumizi ya dawa za fungus (Kuvu) kutoka Kenya kwa sababu za kiusalama

Mamlaka husika ya Afya nchini Rwanda imetaka kurudishwa dawa aina ya antifungal zilizo katika muundo wa vidonge zinazotumika kutibu matatizo ya fungus (Kuvu) zinazozalishwa nchini Kenya kutokana na masuala ya usalama.

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda (RFDA) imewaagiza wazalishaji kurudisha bechi zote za tembe za Fluconazole zenye miligramu 200 zilizotengenezwa na kampuni ya Universal Corporation ya Kenya. Wauzaji wa reja reja na vituo vya afya wametakiwa kusitisha usambazaji na kurejesha dawa hizo za fungus zilizoathirika.

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda RFDA imeagiza hilo kufanyika baada ya kuieleza Kampuni Mzalishaji ya Kenya kuhusu dawa hizo kubadilika rangi bechi nne za vidonge vya rangi ya pink (waridi) vya Fluconazole vya miligramu 200 vilivyoingizwa Rwanda vimeonekana kubadilika rangi na kuwa nyeupe hata kabla ya kumalizika muda wa matumizi stahiki ya dawa hizo.

Vidonge vya kutibu kuvu (Fungus)

RFDA imesisitiza kuwa baadhi ya dawa hizo za kutibu kuvu tayari zimeingizwa sokoni huko Rwanda. Maafisa wa Rwanda wameanzisha uchunguzi ili kubaini iwapo dawa hizo tajwa zina athari mbaya kwa watumiaji au la. 

Wakati huo huo Mamlaka husika za Kenya hadi sasa hazijaeleza lolote iwapo dawa hiyo ya Fluconazole ambayo hutumika pakubwa kutibu fungus (Kuvu) zitaondolewa sokoni au la. 

Tags