MSF: Theluthi moja ya waliojeruhiwa vitani huko Sudan ni wanawake au watoto wadogo
(last modified 2024-07-17T13:09:21+00:00 )
Jul 17, 2024 13:09 UTC
  • MSF: Theluthi moja ya waliojeruhiwa vitani huko Sudan ni wanawake au watoto wadogo

Baada ya kupita zaidi ya mwaka mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan, karibu theluthi moja ya waliojeruhiwa ni wanawake au watoto walio na umri wa chini ya miaka 10. Ripoti hii imeelezwa na Shirika la Misaada ya Kimatibabu la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF).

Umoja wa Mataifa umeitaja hali ya mambo ya sasa nchini Sudan kuwa moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya karibuni. 

Pande mbili zinazozozana huko Sudan zimeshutumiwa mara kwa mara kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kushambulia maeneo ya makazi na kuwalenga raia.

Dr Christou Christos Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kimatibabu la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) ameeleza kuwa wanayatolea mwito mashirika mengine hasa taasisi za Umoja wa Mataifa kurejea na kuchukua hatua zaidi za kuwasaidia waathirika wa vita huko Sudan hivi sasa ambako hakuna ishara yoyote ya kusimamishwa vita nchini humo. 

Drm Christou Christos 

Amesema kuwa makundi mengi ya misaada ya kibinadamu yameripoti kukabiliwa na changamoto za kifedha ikiwa ni natija ya ufadhili duni kwa Sudan suala ambalo Martin Griffiths Mkuu wa masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa  amelitaja  kuwa ni "aibu kihistoria". 

Makundi mengi ya misaada ya kibinadamu yamefanikiwa kutuma misaada katika maeneo yale ambayo yanadhibitiwa na jeshi huko Sudan; huku Umoja wa Mataifa ukizituhumu pande zote mbili zinazopigana kwa kukwamisha upelekaji wa misaada nchini humo.  

Tangu vita vianze huko Sudan hadi sasa jeshi na wapinagaji wa RSF wametuhumiwa kwa vitendo vya uporaji,  kuzuia misaada, pamoja na kuharibu mfumo wa afya ambao tayari ni dhaifu.

Tags