Aug 10, 2024 02:32 UTC
  • Maandamano ya kulaani jinai za Israel yaendelea kufanyika nchini Morocco

Maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na jeshi la Israel huko Gaza.

Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walipiga nara za kulaani mauaji ya umati na jinai zinazofanywa na utawala pandikizi wa Israel dhidi ya raia wa Palestina na kuitaka jamii ya kimataifa kutekeleza wajibu wake wa kuokoa maisha ya raia.

Maandamano hayo ni muendelezo wa upinzani wa wananchi wa Morocco dhidi ya jinai za Israel huko katika Ukanda wa Gaza.

Siku ya Alkhamisi pia maelfu ya wananchi wa Morocco walifanya maandamano na kukusanyika mbele ya jengo la Bunge la nchi hiyo huko Rabat, mji mkuu wa nchi hiyo, kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yamekuwa yakifanyika katika mataifa mbalimbali duniani

 

Maelfu ya wananchi wa Morocco wamekuwa wakifanya maandamano ya mara kwa mara katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani jinai zinazoendelea kufanywa na jeshi la Israel huko Gaza.

Waandamanaji nchini Morocco wamelaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa kuwatesa kwa njaa, kuwazingira kila upande na kujaribu kuwahamisha kwa nguvu watu wa Ukanda wa Ghaza.

Kadhalika wananchi wa Moroco wanaishinikiza pia serikali ya Rabat kufuta makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala katili wa Israel.

Tags