Kiongozi wa Sudan: Mataifa ya kikoloni yanachochea migogoro Afrika
(last modified Mon, 13 Jan 2025 10:49:35 GMT )
Jan 13, 2025 10:49 UTC
  • Kiongozi wa Sudan: Mataifa ya kikoloni yanachochea migogoro Afrika

Kiongozi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al Burhan amesema kuwa mataifa ya kikoloni yanachochea migogoro mbalimbali barani Afrika.

Jenerali Abdel Fattah al Burhan ambaye ni Mkuu wa baraza la Uongozi la Sudan amebainisha haya katika mkutano na Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo katika ikulu ya Rais mjini Bissau. 

Baraza la Uongozi la Sudan limeeleza kuwa Al Burhan na Embalo wamekuwa na mazungumzo ya pande mbili kujadiliuhusiano kati ya nchi mbili na njia za kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali. 

Abdel Fattah al Burhan pia alimweleza Rais wa Guinea Bissau hali ya mambo ya Sudan kufuatia uasi ulioongozwa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) chini ya uongozi wa Hamdan Dagalo. 

Kamanda Dagalo katikati mwenye fimbo na wapiganaji wake wa RSF

Aidha amesema kuna mataifa ya kikoloni ambayo yanatekeleza njama ili kuchochea migogoro barani Afrika. 

" Bara la Afrika linashuhudia vuguvugu la mwamko unaoliwezesha kukabiliana na uingiliaji wa nchi ajinabi katika masuala mbalimbali ya nchi hizo", amesema Kiongozi wa Sudan.

Katika mazungumzo hayo huk Bissau, Rais Embalo pia amesema anatumai kuwa amani itarejea haraka huko Sudan.

A;Burhan aliwasili nchini Guinea-Bissau jana Jumapili akiwa katika ziara yake ya pili ambapo ya kwanza alianzia huko mali siku ya Jumamosi na kuzitembelea pia Sierra Leone na Senegal.