14 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Namibia
Wafanyakazi 11 wa Idara ya Huduma ya Marekebisho ya Namibia, afisa wa polisi na raia wawili wamepoteza maisha jana Jumamosi katika ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la kusini-kati nchini humo.
Rais Netumbo Nandi- Ndaitwah wa Namibia amesema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya magari kugongana uso kwa uso kwenye barabara kuu ya B1 karibu na Mariental, maili 167 kutoka mji mkuu wa taifa hilo wa Windhoek.
"Natoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kwa wanaume na wanawake wa Idara ya Huduma ya Marekebisho ya Namibia na kwa polisi ya nchi hiyo ambao wanawaomboleza wenzao.
Ajali hiyo ya jana huko Namibia ilihusisisha na gari moja na gari la polisi aina ya Van ambalo lilikuwa limewabeba watu sita; watano kati yao wakiwa ni maafisa, raia mmoja na mfanyakazi mmoja wa Idara ya Huduma ya Marekebisho ya Namibia. Gari hilo lilikuwa na jumla ya watu 13. Watu watatu wamejeruhiwa vibaya na wamelazwa hospitali wakiendelea kupatiwa matibabu.