Rais wa Somalia: Somaliland inashirikiana na Israel dhidi ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i134968-rais_wa_somalia_somaliland_inashirikiana_na_israel_dhidi_ya_wapalestina
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amezinukuu ripoti za kiitelijinsia na kusema kuwa eneo lililojitenga la na nchi hiyo la Somaliland limekubali kuwapokea Wapalestina na kuanzishwa kambi ya kijeshi ya Israel katika eneo hilo mkabala wa kutambuliwa rasmi na Israel.
(last modified 2026-01-01T11:23:18+00:00 )
Jan 01, 2026 02:26 UTC
  • Rais wa Somalia: Somaliland imekubali kuwapa makazi Wapalestina
    Rais wa Somalia: Somaliland imekubali kuwapa makazi Wapalestina

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amezinukuu ripoti za kiitelijinsia na kusema kuwa eneo lililojitenga la na nchi hiyo la Somaliland limekubali kuwapokea Wapalestina na kuanzishwa kambi ya kijeshi ya Israel katika eneo hilo mkabala wa kutambuliwa rasmi na Israel.

Rais wa Somalia ameiambia televisheni ya al Jazeera ya Qatar kwamba hatua ya Tel Aviv ya kulitambua eneo la Somaliland haikutarajiwa na ni ya kushangaza. Amesema, Israel ni utawala wa kwanza kuitambua Somaliland kama taifa huru tangu mwaka 1991. 

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 kufuatia vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe lakini haijawahi kutambuliwa rasmi na nchi yoyote mwanachama wa Umoja wa Mataifa. Jamhuri hiyo iliyotangaza kujitenga na Somalia imeanzisha sarafu yake, bendera na bunge, ingawa maeneo yake ya mashariki yameathiriwa na mzozo.

Mogadishu imepinga madai hayo ya kuwa taifa huru Somaliland na kusema kuwa eneo hilo ni sehemu ya Somalia. 

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema kuwa wamekuwa wakifanya jitihada za kuliunganisha taifa kwa njia ya amani. 

Amesema, Somaliland pia imekubali kujiunga na Mkataba wa Abraham uliosainiwa mwaka 2020 kati ya Israel na Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco ili kuhuisha uhusiano. 

"Utawala wa Israel unataka kudhibiti njia za kimkakati za baharini za Pembe ya Afrika na kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina kutoka Ghaza na kuwapeleka Somaliland. 

Mijibizo na radiamali mbalimbali kikanda na kimataifa zinaendelea kutolewa kufuatia hatua ya Israel ya kuitambua rasmi Somaliland huku nchi nyingi zikiitaja hatua hiyo kuwa kinyume na sheria za kimataifa na ni tishio kwa uthabiti wa kikanda.