Mkuu wa upinzani Gabon ataka kufanyika mgomo wa nchi nzima
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14689-mkuu_wa_upinzani_gabon_ataka_kufanyika_mgomo_wa_nchi_nzima
Jean Ping kiongozi wa upinzani nchini Gabon leo ametoa wito wa kufanyika mgomo wa nchi nzima dhidi ya kile alichokiita kuwa ushindi wa kuingia tena madarakani kwa udanganyifu kwa Ali Bongo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 05, 2016 09:29 UTC
  • Mkuu wa upinzani Gabon ataka kufanyika mgomo wa nchi nzima

Jean Ping kiongozi wa upinzani nchini Gabon leo ametoa wito wa kufanyika mgomo wa nchi nzima dhidi ya kile alichokiita kuwa ushindi wa kuingia tena madarakani kwa udanganyifu kwa Ali Bongo.

Ping ambaye amesema yeye hivi sasa ndiye kiongozi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika inayozalisha mafuta amebainisha kuwa, mapambano yake hayajamalizika, hata kama hali ya utulivu imerejea katika mji mkuu Libreville baada ya ghasia kubwa za wiki iliyopita. Jean Ping amewataka wananchi wa Gabon kutotumia mabavu bali amewasihi kuendeleza mapambano kwa kukwamisha uchumi wa nchi hiyo. Amesema anawataka wananchi kusitisha shughuli zote na kuanza mgomo wa nchi nzima.

Jengo la Bunge la Gabon lililochomwa moto na wafuasi wa upinzani waliolalamikia matokeo ya uchaguzi wa Rais

Watu wasiopungua sita wameuawa na wengine zaidi ya elfu moja wametiwa mbaroni kwenye machafuko yaliyoikumba Gabon baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Rais ambapo Ali Bongo aliibuka na ushindi. Ali Bongo amekanusha madai ya kuchakachua kura katika uchaguzi wa rais uliofanyika wiki iliyopita huko Gabon.