Marekani: Hatutaki Riek Machar arejee madarakani nchini Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14890-marekani_hatutaki_riek_machar_arejee_madarakani_nchini_sudan_kusini
Serikali ya Marekani imeweka wazi azma yake ya kutofurahishwa kurejea madarakani kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 08, 2016 09:37 UTC
  • Marekani: Hatutaki Riek Machar arejee madarakani nchini Sudan Kusini

Serikali ya Marekani imeweka wazi azma yake ya kutofurahishwa kurejea madarakani kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar.

Hayo yamesemwa na Donald E. Booth, mjumbe maalumu wa Marekani nchini Sudan Kusini katika kikao cha masikilizano cha baraza la wawakilishi nchini humo na kusema kuwa, kwa kuzingatia mwenendo wa machafuko ambayo yamekuwa yakijiri Sudan Kusini, Riek Macha hatakiwi tena kurejea katika nafasi yake ya makamu wa rais. Hata hivyo Booth ameongeza kuwa, kutorejea madarakani Riek Machar hakutakiwi kutumiwa na Rais Salva Kiir kama wenzo wa kuwakandamiza wapinzani wake.

Riek Machar makamu wa zamani wa rais wa Sudan Kusini

Aidha amemtuhumu Rais Kiir na Machar kwamba baada ya kutiliana saini makubaliano ya amani, wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa ajili ya kuanza hatua za utekeleza makubaliano hayo ili kukomesha mapigano nchini na kwamba pande mbili hizo zimeshindwa kabisa kuwadhibiti wafuasi wao kunako suala hilo. Mvutano wa kisiasa baina ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka na Riek Machar wa kabila la Nuer, ulianza tangu miaka mitatu iliyopita, mivutano ambayo ilizivuta pande hizo kuingia katika vita vya ndani vilivyosababisha mauaji ya maelfu ya watu na wengine wengi kuwa wakimbizi. Riek Machar alikimbilia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kisha Sudan hivi karibuni, baada ya kushtadi mapigano mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.