Wapinzani Kongo DR wasusia mazungumzo ya kitaifa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15934-wapinzani_kongo_dr_wasusia_mazungumzo_ya_kitaifa
Wapinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesusia kushiriki kikao cha mazungumzo ya kitaifa.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Sep 24, 2016 04:36 UTC
  • Wapinzani Kongo DR wasusia mazungumzo ya kitaifa

Wapinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesusia kushiriki kikao cha mazungumzo ya kitaifa.

Ripoti kutoka Kinshasa zinaarifu kuwa Vital Kamerhe mwakilishi wa mrengo wa upinzani katika mazungumzo ya kitaifa ya Kongo yanayofanyika ili kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo amesema kuwa ameahirisha kushiriki mazungumzo hayo ili kulalamikia ghasia zilizosababisha vifo vya raia wa nchi hiyo huko Kinshasa. Mazungumzo ya kitaifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo yaliakhirishwa hadi siku ya Jumanne,  yalitazamiwa kuanza tena Ijumaa ya jana asubuhi, hata hivyo baadaye iliamuliwa kuwa mazungumzo hayo yaakhirishwe hadi wakati mwingine kwa kuzingatia hali ya mambo ya Kongo. 

 Hii ni katika hali ambayo Kanisa Katoliki ambalo lina heshima nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na nafasi yake kuu katika kuanzisha mchakato wa demokrasia katika mungo wa 90, Jumanne iliyopita pia lilisusia mazungumzo ya kitaifa ya nchi hiyo.  Ghasia na machafuko yalijiri pambizoni mwa maandamano ya wapinzani  mwanzoni mwa wiki hii huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo na kusababisha makumi ya vifo vya watu.

Polisi wakikabiliana na raia mjini Kinshasa